Natangaza rasmi kujiunga CCM

Changamoto ni watanzania hatujui kuchambua mambo na kuyahusisha na maisha yetu.

mifumo yetu ya elimu haituwezeshi kuoanisha practical life na theorical knowledge.

anayekabiliwa na changamoto sio chama cha mapinduzi bali ni watanzania.

chama cha mapinduzi hakina mwenyewe bali ni mali ya watanzania.

ni sawa na watanzania tulivyounda mashirika kama tanesco kushughulikia mambo ya umeme. sasa kama tumeunda shirika la tanesco tukakusanya kodi tukaweka na wakatokea baadhi ya watanzania wakagundua kuwa watanzania tumelala wakatumia kodi zetu tunazoingiza tanesco kwa matumizi yao na sisi tukabaki tukisema tatizo la tanesco ni kutokuboresha umeme hivyo bora yaje makampuni ya kigeni yatupatie umeme unadhani nani mjinga hapo je ni wale wachache waliotuibia? au ni sisi wenyewe tulioibiwa tuna matatizo?

mfumo wetu wa siasa tumeweka uongozi wa nchi lazima upitie kwenye vyama vya siasa. asilimia kubwa ya watanzania tumelala lakini wakawepo wahuni wachache wakatutambua tulivyolala wanaingia wanasimama kwenye majukwaa wanatulaghai kwa maneno kwa staili ya matapeli tunawakabidhi madaraka kumbe wengi si viongozi.


tukitambua hili hatutakaa kuangalia jina la chama na kudhani jina ndio tatizo, kama unavyoona mkisema kampuni haitalipa kodi miaka mitano na wajanja wakaanza kubadili majina na kujifanya ni kampuni mpya na kuendelea kutokulipa kodi ndivyo wajanja hawa watakavyobadili majina ya vyama lakini matendo ni yaleyale na watu ni walewale.

tunahitaji kutambua matatizo yetu ni yapi na tutatue hayo na sio kukalili majina ya makundi kumbe wajanja wanahama huku na kule.

 
ni lazima tujiulize hapa tulipo tunahitaji nini?
 
Kama jinsi Kikwete na CCM walivyo athiri maisha ya watanzania kwa asilimia 75, ni upumbavu na ujuha kuamini ahadi za CCM, kuwa ccm na magufuli wataleta maendeleo waliyoyashindwa kwa zaidi ya miaka 50.
 
Mimi mwana CCM Kindakindaki naapa kuwa nitampigia kura EDWARD NGOYAI LOWASSA anayeiwakilisha CHADEMA kupitia mwamvuli wa Muungano wa vyama vya UKAWA. Kama kuna wakati ambapo CCM inahitaji kujipanga vyema na kurekebisha mapungufu yaliyopo wakati huo ndio sasa.Kwa yeyote anayeipenda CCM kama mimi,naomba kwa Moyo Mkunjufu tuiweke CCM pembeni ili ikajikague,ikajitafakari na kisha ijipange kwa ajili ya 2020 - 2025.Gari ama mashine yeyote ile hata iwe "tingatinga" ikiharibika sharti iwekwe pembeni ili ifanyiwe marekebisho muhimu.Ukiilazimisha iendelee na kazi ama iendelee na safari madhara yake ni makubwa sana kwa abiria,mazingira na hata watu waliokaribu na mashine hiyo!!Kataa vitisho,kataa kununuliwa kama bidhaa,kataa uchochezi,kataa ahadi hewa zisizotekelezeka,kataa michezo michafu ya Kisiasa...Jiandae kupiga kura yako kwa Diwani,Mbunge na Rais wa UKAWA.....MUNGU ibariki TANZANIA na watu wake wote!!
 
Katiba inakuruhusu wala hukua na haja ya kututangazia.
 
unachotakiwa kujua ni kuwa vyama vya siasa ni taasisi ambazo mtanzania yeyote anaweza kujiunga na kujitokeza kuwania uongozi wa nchi hii. katika hilo utagundua kuwa ni vigumu kuwatambua watu kama wanawafaa wananchi au hawawafai kwa maana hakuna anayesimama jukwaani kusema mimi nitafanya mabaya.

hapo ndipo inapobidi twende mbali zaidi na kutafuta mbinu ya ziada ni jinsi gani tunaweza kupata yale tunayoyataka kutoka kwa viongozi wetu.

ndipo tunaporudi nyuma na kujiuliza hivi CCM unaowalaumu kabla ya kuwapa kura waliongea tofauti na hao unaowaona leo mashujaa wako? utasema na wao mda wote wamekuwa wakiongea kwa machungu yaleyale na kwa mbwembwe zile zile lakini uzoefu umeonyesha kuwa wapo wanaotenda tofauti na wanayoyasema kwenye majukwaa.

hapo ujiulize tabia hiyo je ina itikadi au katika jamii wapo wanaosema mambo wakayatekeleza na hawa ndio wanastahili kuwa viongozi na wapo wanaosema ngonjera tu majukwaani ili kupata uongozi na wakipata uongozi wanafanya ya kwao.

utagundua tabia hii ni ya wanadamu wenyewe na hawa wanapokuwa wanaingia kwenye vyama hawana mchujo hivyo kila chama kina tabaka zote mbili.

lakini vyama hivi vinatofautishwa na uzoefu kwa maana chama kilichokaribisha watu wakakaa pamoja, wakaongea lugha moja kwenye majukwaa lakini katika utendaji wakatofautiana kinakuwa na uzoefu ambao kinaweza kuwabaini watu wakweli miongoni mwao na kuwaweka mstari wa mbele na waongo kuwaweka kando au kinyume chake kwa maana uongo na ukweli mara nyingi havikai pamoja kwa kuwa maslahi yake yanakinzana.

hivyo ccm si mali ya mtu fulani ni taasisi yetu watanzania inayotumika kututafutia viongozi wanaofaa. ni wajibu wetu watanzania kuzielekeza taasisi hizi zitutumikie mda wote na sio kuziacha wanaingia wahuni wanatuibia na kuondoka na sisi tunabaki kudhani taasisi zenyewe ndio mbaya. yaani kama tuna shirika akapewa kiongozi akatuibia na sisi tukabaki kukariri kuwa shirika ndilo baya lakini aliyetuibia mzuri sidhani kama tunakuwa tumelitafakari hili vizuri.

sio ccm tu bali taasisi zote za kutuletea viongozi zinatakiwa kwanza ziwe za kitaifa na sio za watu binafsi na tuzielekeze kutupatia viongozi bora.

ukifuatilia kinachotendeka katika nchi yetu na kilichofanyika katika ccm katika uchaguzi huu nashindwa kuelewa kwa nini bado ukilaumu chama hiki badala ya kuangalia kuwa kazi kubwa imefanyika ya kujaribu kurekebisha makosa.

asiyeweza kutafakari jinsi tunavyokwenda ndiye anayedhani ni bora kurudi kwenye hatua za miaka ya 60 ya kusikiliza kelele za watu majukwaani bila ya kwenda mbali ya hapo na kufanya uchambuzi wa kina.

wapo watu ndani ya vyama vidogo hivi vinavyokua ambao wanajua kuwa wakipewa madaraka leo nchi itarudi nyuma lakini kwa ubinafsi wao wa kuweka vyama vyao mbele ili vikue na kwao njia hiyo ndiyo inawapa maslahi makubwa zaidi wanakaa kimya na kutumia mtaji wa ujinga wa majority kujinufaisha.

ni jukumu la watanzania kuangalia wanapata faida wapi na wafanye maamuzi kulingana na faida.

katika kazi yoyote ukimchukua fundi aliyetoka shule hajawahi kufanya kazi yoyote wakati mwingine anakuwa na majigambo mengi lakini akifikiria nadharia zaidi kuliko vitendo. vyama vidogovidogo vinachukua watu wengi ambao hawajawahi kuongoza kitu chochote au wasiojua mifumo kabisa ya utendaji wa serikali na hawa wanasimama kwenye majukwaa wakikosoa lakini wengi wao wakiwa hawajui hata la kufanya pia.

fundi mzoefu anaweza kuwa amewahi kufanya makosa mengi lakini makosa na mambo aliyofanikisha yanamfanya awe na uzoefu wa kufanya vizuri zaidi.

hivyo chama chenye wigo mpana wa kuchanganya vizazi tofauti katika utawala wake kinakuwa na nafasi nzuri ya kuipeleka jamii mbele kwa kasi.

huko nyuma ccm walikuwa wazee wakigangania madaraka na walipokuwa wakipitwa na wakati walijikuta serikali ikitembea nyuma huku wananchi wakiwa mbele yaani kiongozi yuko nyuma na wanaoongozwa wako mbele. hii ilibadilisha jukumu la serikali kutoka kuwa kiongozi na kuwa kama afisa usalama ambaye anaagalia nani kakosea kuadhibu na sio kuwaelekeza watu nini wafanye.

baada ya ccm kujitafakari wamebadilika na kuanza kuchanganya vizazi ingawa upendeleo bado unadidimiza kasi ya maendeleo.

vyama hivi vinaonekana kuikosoa ccm bila kujua ccm walijikwaa wapi hivyo wanafanya yaleyale huku wakiwakosoa. jiulize sababu zilizofanya viongozi wa ccm washindwe kutimiza tunayoyaona na ujiulize hawa wanambinu gani kuyaepuka?

mfano angalia serikali inavyopata watendaji katika nyadhifa muhimu na urudi kwenye vyama hivi uangalie mfano uteuzi wa wabunge wa viti maalumu je wanafanya yaleyale au wao ni tofauti?

kiongozi bora katika nchi hii hawezi kuanzia kwenye kutupatia mahitaji bora bali ataanza kurekebisha mifumo ya nchi na mifumo hii ndiyo itatoa huduma bora kwa watu. tunataka kiongozi ambaye anawajali watu atengeneze mifumo ambayo daima akija kiongozi mbovu mifumo inamkataa au inamrudisha kwenye uzuri yaani viongozi wategemee mifumo nasio mifumo kutegemea viongozi.

ni mtu gani tunayemuona katika waliojitokeza kuwa na nia ya dhati, kuwa na uwezo wa kurekebisha mfumo, kubadilisha hulka na tamaduni mbaya.

Kama jinsi Kikwete na CCM walivyo athiri maisha ya watanzania kwa asilimia 75, ni upumbavu na ujuha kuamini ahadi za CCM, kuwa ccm na magufuli wataleta maendeleo waliyoyashindwa kwa zaidi ya miaka 50.
 
(Sorry offtopic)
NI STRATEGY NZURI SANA YA KUPATA REPLIES........
 

Attachments

  • QWQ.JPG
    77.6 KB · Views: 532
Mahubiri marefu yasiyo na mantiki, it wont change reality kuwa CCM wameshindwa kuleta maendeleo. PERIOD.

Hata wakishinda kwa hila, still tutaendea na shida hizi hizi. CCM sio mtu sisi ni taasisi kama ulivyosema( Tafadhali ondoa hilo neno kuwa nitaasisi yetu watanzania).

Kilichoshindwa kuleta maendeleo ni taasisi CCM, sasa Magufuli anatushawishi kuwa ataleta maendelo kupitia hiyo taasisi iliyoshindwa na atatumia watendaji wale wale walioshindwa ambao anapita kila mahali kuwanadi ili warudi kuendesha taassis hiyo hiyo. Nikweli kabisa inabidi uwe na akili fyatu kidogo ili uweze kuamini Taasisi CCM.

Sina shida na magufuli, ni mchapa kazi. lakini taasisi CCM anayo jinadi nayo imeshindwa kutuleta maendeleo, wachache walio kwenye mfumo ndani ya taasisi wamejineemesha wao na watoto wao na vizazi vyao.

Tunajua kweli kabisa Lowasa sio safi na hata Mbowe pia lakini je ninani ndani ya CCM alie msafi? je wachafu walio ndani ya CCm si ndio wengi kuliko chama chochote kile? Mnaimba kuwa Magufuli ni muadilifu, je mnaelewa uadilifu ni nini? Mnaangalia boroti katika jicho la wenzenu lakini ninnyi mko na kibanzi hamtaki kukiangalia.

Kama Taasisi CCM ilifanya mema kwa wananchi, kwanini inatumia nguvu kubwa sana kujiuza kwa wananchi? kama taasisi CCM ingekuwa kwa muda wote wa utawala wake ( sio uongozi) imefanya mambo mazuri kwa wananchi, isingehitaji kutoa ahadi ili ipewe kura, ingetuambia "mmeona hiki na hiki tulichofanya? tupeni kura ili tuendelee kuwaletea maendeleo".
Lakini CCM imekuwa ikitoa ahadi kama vile ni chama kipya katika nchi huku ikiwashawishi wananchi wakiamini na wakipe kura.
 
nahitaji kadi ya ccm ya uana chama, taratibu zake zipoje na gharama zake na naipata wapi
 
Heri yako wewe umejielewa mimi huku njaa tuu ndio inanikalisha ila 25 october Magufuli oyeeeeee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…