Natangaza nia ya kugombea Ubunge 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natangaza nia ya kugombea Ubunge 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by elly1978, Jan 20, 2012.

 1. e

  elly1978 Senior Member

  #1
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 180
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mimi ni mtanzania wa upande wa Bara, nataka kugombea ubunge wa bunge la jamhuri ya muungano kwa tiketi ya CUF, jimbo la uzini, zenji, wadau inawezekana?
   
 2. H

  Haki sawa JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 3, 2007
  Messages: 4,701
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Hakuna nafasi kama hiyo imetangazwa kuwa unaweza kugombea ubunge wa uzini , ila ni kuwa mjumbe wa baraza la wawakilishi , kitu ambacho sio cha Muungano.

  Unazijua sheria za uchaguzi Zanzibar? zijue kwanza kabla ya kuandika ulichoandika
   
 3. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2012
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,211
  Likes Received: 3,625
  Trophy Points: 280
  Kasema atagombea mwaka 2015 na wala sio sasa na ana haki kugombea kikatiba Ubunge jimbo lolote la Ubunge TZ likiwemo la Uzini kwani sifa pekee unayotakiwa kuwa nayo ni kuwa Mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18!

  Ila huwezi kuwa na sifa ya kugombea Ujumbe wa Baraza la Uwakilishi hasa kama unaishi Bara kwa sababu sifa kuu ya kuteuliwa ni lzm uwe na ID inayoonyesha ww ni mkazi wa Zanzibar at least kwa miaka 3 mfululizo!

  Jimbo hilo mbunge wake ni Mzee Seif Khatib(Correct me if i'm wrong)na "mwenye nalo Mzee Khatibu"sijasikia kama katangaza kung'atuka!
   
 4. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,437
  Likes Received: 1,018
  Trophy Points: 280
  Ngoja wakutoe kishipa, jamaa ni wabaguzi sana
   
 5. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Unataka kugombea Ubunge au Uwakilishi?
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Jan 20, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Dini gani wewe?
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Jan 20, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Hilo jina la Elly linadhihirisha wewe si mtoto wa mamdogo. Watoto wa mamdogo ndiyo wenye nafasi ya kushinda zenji. Mambo ya Bwana asifiwe kule akaa!!
   
 8. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kama wewe ni mtanganyika na kweli uko serious ni heri ujipange ugombee majimbo ya bara
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu unachokonoa Muungano!? Nawakumbuka wachache: Kisasi na Mwakanjuki lakini nao nadhani walizaliwa visiwani. Sasa kama wewe ni wa mrima basi huna chako huko Uzini, Wawi, kibandamaiti, Kojani, Mjimkongwe wala Makunduchi! Chao chao chetu chao!
   
 10. e

  elly1978 Senior Member

  #10
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 180
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kumbe dini nayo yatakiwa, mimi na mkristo mkatoliki
   
 11. e

  elly1978 Senior Member

  #11
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 180
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ya bara wapiga kura wengi, nimegundua zenji kura elfu 2.5 nimeshaingia mjengoni, kupiga kampeni itakuwa rahisi kwangu maana sina fedha za kutosha.

  Si kuna wazenji wanawakilisha majimbo ya Bara kule Dom? Au sisi watanganyika haturuhusiwi kugombea kwao ila wao ruksa kwetu?
   
 12. monongo

  monongo JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 370
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Zenji cio Tanganyika bali ni usultanini, huko hakuna samahani, bali ni jicho kwa jicho, na jino kwa jino.bora nguvu hiyo uihamishie huku kwenu!!(wabaguzi sana wa Itikadi, hapafai)
   
 13. knownless

  knownless Senior Member

  #13
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 116
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  nimeona sifa mbili ambazo kwa hakika hutofanikiwa kutimiza malengo yako.
  1. Utanzania Bara. Mpaka hapo umeshashindwa kwani hao jamaa kwa ubaguzi hawafai,hiyo itakuwa point of weakness ambayo wapinzani wako wataitumia kukumaliza kwenye kampeni.
  2. Dini. Wewe kuwa mkatoliki ni kigezo tosha kukumaliza. Huko zenj wakristo hawatakiwi sema basi inabidi wajizuie tu,mfano makanisa kuchomwa moto bila wahusika kuchukuliwa hatua zozote.

  Kulingana na hizo sababu kuu mbili wala usijisumbue kugombea huko nchi ya jirani kwani utapoteza tusenti twako na muda utakao tumia kipindi cha kampeni.
   
Loading...