Kuna rafik yangu alikua na mke, mke alikua hapumziki hata kuongea na simu ilifika wakati akavunja dirisha la chumbani kwake na simu zote pamoja na ya kwake akaiiba, alipata mapumziko kidogo, lakini alinifurahisha aliponiambia mke wake akimuaga anataka kwenda kwao jambo la mwanzo hukimbilia chooni kwenda kufurahi.......
kumbe mnajua zinachosha eeeh???? halalisheni ndoa za mikataba sasampeane likizo jamani angalau mmisiane. kukaa na mtu miaka nenda rudi nayo inachosha.
Ni wakati mwafaka kuwekeza katika ndoa (na si sherehe za ndoa)kwa muda ,mali,na akili zetu!Ndoa nyingi zina shida, zinaumwa, zimechoka na zipo kwajili tu ya mazoea (tunaishi basi tu),watoto hawana tena malezi mema, haipiti wiki bila kununiana japo kwa muda (mnapeana half time).
Juzi katika pilika zangu za maisha ndipo tukiwa tunafanyiana counselling mmoja wa victim akasema kwa maumivu makali snaa kuwa, angetamani sana japo mpenzi wake (female/male??) asafiri apumue kidogo....Mapenzi yanapofikia huku, ni kipindi cha kila mmoja kuonyesha misimamo positive, kukimbia, kusafiri, kumuombea msiba/kifo au kuwa na KIDUMU hailipi hata kiduchu.
Kama mwaka 2012 ulikua mwaka wenye matatizo na changamoto katika familia, basi 2013 ni muda wa kurekebisha, yaache na kuyasahau yaliyopita, na MUNGU wangu awapiganie muwe na NDOA takatifu na kuwalea watoto katika malezi bora.
Ona mifano hii, wewe je nini uzoefu wako? Sizungumzii GF na BF please
Mkishafikia huko chukueni break, yaani tenganeni ikibidi kusafiri holiday pekeyao ili kung'amua uwekezekano wa kuwa pamoja tena au kuachana kabisa.
Lakini kwa waafrika hii kitu haipo kupeana break
kuna wenginme wanakuaga uso wa mbuzi milele...kikubwa ni maombi tu yatasaidia japo kidogoCold Wars hizi ni mambo ya kawaida sana. Inaweza kupita wiki kila mtu kivyake baadae inakua fresh especially kama mna watoto at some point mnaanza kuwasiliana.
Ni wakati mwafaka kuwekeza katika ndoa (na si sherehe za ndoa)kwa muda ,mali,na akili zetu!
Mimi nilifikia wakati nikatamani acheat ili aniwache NIPUMUWE!
Married and bored or Single and lonely.
Watu wengi wanaoa kuridhisha jamii zinazowazunguka inaonesha kama ni right thing to do at a certain age.
Kwa hiyo unapumua sasa au unatumia oxygen (mipira puani).
Mkishafikia huko chukueni break, yaani tenganeni ikibidi kusafiri holiday pekeyao ili kung'amua uwekezekano wa kuwa pamoja tena au kuachana kabisa.
Lakini kwa waafrika hii kitu haipo kupeana break
hahahhaaaa una utani na watu wewe? tena asubuhi asubuhi namna hii
Siku zote silaha yangu kubwa kuendelea kuwa na amani na furaha, ni kujifunza kusamehe na kusahau...Ni ngumu lakini inawezekana
Haha sasa naona leo kila mtu anatoa ushuhuda wake moyoni, mie huwa nakaa kimya kabisa, hata aniongeleshe vipi najizuia nisimjibu, anajua vyema but then tunaendelea vziru tu, huwa nasamehe on spot wakati anaongea ndio maana huamua kukaa kimya nisijibishane nae
Mpwa ni kweli kabisa, sio kweli mara zote akina Mama wako negative kwa kila kitu , No No, hawa watu resource nzuri sana ya kila kitu. Unakaaa kimya kwa vitu ambavyo labda unaona ukiongea itakua purukushani kubwa zaidi sasa ili kuzuia hayo yote unakaa kimya halafu unajua nini asubuhi kukipambazuka namtekenya kidogo, mwanzoni ilikua ngumu but now amezoea kuwa tukishatofautiana kitakachofuata kesho yake ni tekenyo.....Nimeipenda sana hii, ndio silaha yangu pia, maisha ni mafupi sana kwanini nijipe shida, Hakuna mtu aliye mkamilifu, na isitoshe sitaki kuumiza kichwa changu kwa ajili ya mtu mwingine,Kila Binadamu anayo madhaifu yake .
Elli na mimi napenda sana staili hii, umamuacha anaongea tu baadaye hujikuta anaongea peke yake, na akishaona hivyo anajua kuwa umempotezea , basi asemi kitu tena.Lakini huwa namfuraia sana kwa kuwa anachangamoto nyingi sana,ila jinsi tunavyoishi pamoja najikuta nazidi kumpenda kila siku, nikiangalia strength zake , najiona kuwa na bahati kwa kuwa na mwanamke kama yeye.