Natamani Midahalo ya Nguruma hall na Ubungo Plaza irudi

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Vijana waliojua siasa nyuma ya mwaka 2014 wanakosa uhondo wa majidiliano yenye Afya yaliyokuwa yakiendeshwa na taasisi mbalimbali zakiraia yakihusisha Wataalamu na magwiji mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Nakumbuka Midahalo ya Nguruma hall, hapa zilizaliwa fikra pevu na ndipo walipo zaliwa wafuasi wengi wa UKAWA 2015. Vijana walijengwa kubishana kwa hoja huku wakionyeshwa aina ya Tanzania tuitakayo. Uhuru wakujadiliana ulikuwa mkubwa na ulifanya Taifa lijenge watu wenye confidence yakusimama na kuizungumzia Tanzania ndani na nje.

Nakumbuka mdahalo uliowakutanisha Prof. Sospeter Muhongo na Reginald Mengi kipindi cha vitalu vya gesi. Wazee wale walifuana mmoja akitumia skills za biashara na mwingine akitumia skills za taaluma ya darasani, Mambo haya siku hizi hayapo.

Hii mijadala natamani irejeshwe kupitia Kigoda cha Mwalimu au kupitia taasisi zinazosimamia democracy, kuna Jambo kubwa sana vijana wanapaswa kujifunza kutoka kwa wazee wetu wakina Waryoba, Butiku, Shivji, Ulimwengu, JK, Prof Safari, Baregu, Kabudi nk. Hawa watu ukiwasikiliza wakibadilishana mawazo out sense of politics hutachoka kujiona Mtanzania.

Mh. Rais tufungulie hii mijadala utapata thawabu nyingi na Taifa litapumua.
 
Ni kweli, inabidi tutengeneze lodge houses na house of lords ili tuwe na mijadala....
 
Naunga nkono hoja.

Enzi za JK Nkrumah hall watu walikuwa wanamkoma nyani giladi kwelikweli.

Alivyoingia mwendazake midahalo ikapotea
 
Back
Top Bottom