..........................
Tumekaa kwenye uhusiano kwa muda wa mwaka na nusu sasa mpaka pale mkewe alipokuja kugundua. Mimi mkewe nilikuwa nimeshamjua. Ni mdada msomi na ana kazi nzuri sana ila ni wa kawaida na aniingii hata nusu kwa uzuri kwa hiyo nilijua tu kuwa mumewe atakuwa ananipenda mimi zaidi na labda kuna siku nitakuwa mke wa pili kwani ni muislamu.
Tatizo limeanza miezi miwili iliyopita. Jamaa alinipigia simu akanambia mkewe amejua kuwa tuna uhusiano, kwa hiyo mimi na yeye basi kwani hataki kuvunja ndoa yake. Nimeumia sana imagine mwaka na nusu na nimeshampenda sana. Nimejitahidi kumfuata ofisini kwao secretary wake ananambia jamaa kasafiri wakati gari naliona nje ya ofisi. Nimempigia simu simpati naona amebadili namba.
.....................................
1. mwanadada uzuri pekee si kigezo cha kupendwa zaidi. So futa kabisa akilini mwako eti kisa we ni figure no 8 ndio utapendwa sana.2. Huo ukatili wa wanaume unauovutia upande wako eti!! Vp kuhusu ukatili alioufanya huyo jamaa kwa mke wake? Dont be selfish just stay away from them.3. Naona umeanza hadi kufikiria kumroga mme halali wa mwanamke mwenzako eti. Kwa nini usitulie na kumsubiri wako? Hakuna uchawi mzuri kma kumheshimu mumewe, kumjali na kuongea naye vizuri. Hivyo ndivyo wanawake wengi ambao ndoa zao zinadumu hufanya.4. Acha kumsumbua na kumfuata fuata mme wake hapo ndio huyo mke wake ataacha kukusumbua. Just live ur life and let them live their lives.Ni mdada msomi na ana kazi nzuri sana ila ni wa kawaida na aniingii hata nusu kwa uzuri kwa hiyo nilijua tu kuwa mumewe atakuwa ananipenda mimi Hivi kweli wanaume mnaweza kuwa wakatili hivi? Hivi nyie wanawake wa kwenye ndoa uwa mnawaroga wame zenu? Na huyu mkewe nimfanyeje aache kunifuata fuata. Maana amekuwa ananipa vitisho kila kukicha mpaka nahofia uhai wangu.
na wewe huna maneno mengine ya kumwambia mpaka umuumize au kwa kuwa ana mpango wa kufa?Dada unaonekana umzuri lakini mambo adimu huna hahahahahahhhha,pole kula uzuri huo....umetumiwa kama pedi kwisha khabar yako
oops badilisha number huyo mkewe atakuwa hakupati,kwa kifupi anza maisha yako upya kama vile hujawahi kukutana nao....
Mi sikupi pole hata kidogo.ulipogundua ni mume wa m2 ulipaswa kuachana nae asap,lakini kwa kutumia kigezo cha uzuri uliona uliendelea kujipa moyo ati utakuwa second wife.kwani jamaa aliwai kukutamkia kuwa anataka kuoa tena? Nakushauri futa kabisa iyo mentality ya uzuri kwani ndo inakudanganya.nani alikwambia mwanaume anapenda kwa kuangalia uzuri na figure
Habari zenu wana Jamii Forum. Mimi ni mgeni humu. Ila si mgeni ki hivyo nimekuwa natembelea bila kuwa member. Nimeamua kujiunga ili nipate kushauriwa kwani shida niliyonayo siwezi kushare na mtu ninaye mjua.
Mimi ni mdada wa miaka 32. Ni mrembo sana yaani wale mnaoita 8 figure. Sijisifii ila hilo nimeona nilitamke ili muweze kuielewa vizuri mada yangu.
Nilitokea kumpenda sana kijana mmoja na kuja kugundua baada ya miezi miwili kuwa ni mume wa mtu. Kaka ni muislamu hivyo havai pete na kwa kuwa ni kijana sikuweza kudhania kuwa ni mume wa mtu na kwa kweli ningejua nisinge mpa moyo wangu.
Tatizo niligundua kuwa kaoa wakati nimeshampenda. Na ni yeye mwenyewe alinitamkia kuwa nina mke baada ya kujua sitaweza kumwacha kwani nilikuwa nimekolea.
Tumekaa kwenye uhusiano kwa muda wa mwaka na nusu sasa mpaka pale mkewe alipokuja kugundua. Mimi mkewe nilikuwa nimeshamjua. Ni mdada msomi na ana kazi nzuri sana ila ni wa kawaida na aniingii hata nusu kwa uzuri kwa hiyo nilijua tu kuwa mumewe atakuwa ananipenda mimi zaidi na labda kuna siku nitakuwa mke wa pili kwani ni muislamu.
Tatizo limeanza miezi miwili iliyopita. Jamaa alinipigia simu akanambia mkewe amejua kuwa tuna uhusiano, kwa hiyo mimi na yeye basi kwani hataki kuvunja ndoa yake. Nimeumia sana imagine mwaka na nusu na nimeshampenda sana. Nimejitahidi kumfuata ofisini kwao secretary wake ananambia jamaa kasafiri wakati gari naliona nje ya ofisi. Nimempigia simu simpati naona amebadili namba.
Hivi kweli wanaume mnaweza kuwa wakatili hivi? Kibaya zaidi mkewe kutwa ananipigia simu na kunitisha kuwa atanifukuzisha kazi. Mimi sijali kufukuzwa kazi kwani ninampenda sana huyo mwanaume.
Nishaurini nifanyeje kwa wale wenye uzoefu wa kuwa vimada na wale wenye nyumba ndogo.
Msinitukane jamani. Mimi sijawahi maishani mwangu kutembea na mume wa mtu zaidi ya huyu na sikuwahi kuwaza kuwa yatanikuta. Hivi nyie wanawake wa kwenye ndoa uwa mnawaroga wame zenu? Iweje mtu niliyekuwa nampagawisha the other day leo aseme sitaki kukuona tena kisa tu mkewe kajua?
Na huyu mkewe nimfanyeje aache kunifuata fuata. Maana amekuwa ananipa vitisho kila kukicha mpaka nahofia uhai wangu. Mumewe mwenyewe kesha niacha na yeye bado analeta mikwara wakati nikimwangalia hata ngumi moja namuua.