Ndugu zangu wanajf, natamani siku moja kuiona Tanzania mpya itakayo heshimu haki za binadamu, itakayokuwa na uchaguzi wa haki na huru, itakayo kuwa na vyombo madhubuti vya usalama vyenye uwezo wa kubaina matukio kabla ya kutokea na pale yakitokea utatuzi wa kudumu unapatikana.
Natamani kuiona Tanzania yenye idara imara za serikali zisizoyumbishwa na viongozi wa kisiasa kwa maslahi ya wachache. Natamani kuiona Tanzania yenye kuheshimu na kutekeleza ushauri wa wataalamu wa vitengo mbalimbali. Natamani kuiona Tanzania yenye siasa za kistarabu zisizo na ubabe ambapo mtu akishindwa atakubali kushindwa na kukabidhi madaraka kwa amani. Nadhani Tanzania hii itapatikana kama mimi, wewe na yule tutaamua kwa pamoja bila kujali itikadi zetu za kisiasa, dini zetu na kabila zetu. Eee Mwenyezi MUNGU ingia ndani ya mioyo ya watanzania wote ili tuijenge Tanzania mpya. AMEN.