Natakiwa kuwa mganga

Joined
May 23, 2023
Posts
79
Reaction score
152
Habari

Mwenzenu niliumwa Sana nilienda hospital hawaoni ugonjwa

Hivi juzi Kati nikageukia tiba asilia

Ni huko ndiyo nimeambiwa kuwa ugonjwa wangu hauhitaji dawa Ila natakiwa niwe mganga ndio nitapona

Naomba mnishauri jamani nifanyeje Mimi sitaki kuwa mganga

Au kama kuna vitu ambavyo nikitumia hivi vimahoka vitakimbia naomba mnielekeze
 
Hicho kilichokutokea ni kutokana na kukabidhiwa mikoba ya uganga na mizimu ya kwenu hata kabla hujazaliwa kwa sababu walikuona.

Hakikisha unamjua na kumtumikia Muumba wako maana hiyo mizimu haijakuumba hata ukucha bali inatumia ile haki ya damu nyekundu kusema kwamba wewe ni damu yao.
 

Vimahoka 🤣🤣🤣
 
Hivi kwanini wenye navyo hawawi matajiri😠😠😟
 
Ni kweli uganga sio starehe hata kidogo, kuna mambo mengi ya kutisha na mabaya utatakiwa kufanya bila ridhaa yako. Itabidi ujishike na Mungu wa Kweli kwa nguvu zako zote uepukane na mizimu ya kwenu. Kifupi tu ni kwamba kuwa Mkristo imara mwenye kumwamini na kumfuata Yesu Kristo kwa imani na matendo. Nenda kwa mchungaji wa kweli akuongoze kwenye wokovu wa Yesu Kristo, hiyo ndio dawa pekee ya hayo mambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…