Unajua maana ya ndoa wewe?
Kwanza inavyoonekana mkeo humpendi . eti anachelewesha chai? hiyo nayo sababu? unajua anavyochoka katika kukuhudumia na kulea watoto na kuweka nyumba sawa? mbona hutuambii huwa analala saa ngapi? unafikiri kukaa mtu mama wa nyumbani anakuwa hana majukumu?je umemwekea housegirl na bado hakutayarishii chai mapema?
Sababu zako nyepesi mno... nyie ndiyo mi janaume mnaotelekeza familia zenu kwa kukimbia majukumu...
ulishamuuliza kwanini anakufuata mpaka kazini?utakuwa na mapungufu wewe unajaribu kuona matokeo badal ya kujua sababu.
Na kwa taarifa yako ukimwacha huyo hutapata raha yeyote ya mke na familia katika maisha yako.Mikosi na laana itakuandama..mitafaruku na karaha za magomvi kati ya wanawake wawili uliozaa nao itakukondesha na hautafurahia maisha.Kikubwa muonye Mkeo kwa upendo, kama toka mnaoana hakuwahi kufanya hivyo(miaka ya mwanzo) basi ujue tatizo liko kwako linalomfanya akufuate ofisini...Hakuamini...na wewe si mwaminifu kwenye ndoa