nataka kumshitaki kwa sauti kubwa ya redio!

Linamo

JF-Expert Member
Jan 12, 2011
9,976
24,488
Nawasalimieni JF!

Naomba kusaidiwa nifanyeje kwa huyu jirani yetu?
Yaani yeye asubh ,mchana,usiku anafungulia mziki wake kwa sauti ya juu hapa mtaani ni mziki wake tuuuu!
Hivi hakuna sheria tukamshitaki/nkamshitaki ili ajifunze kwa upuuzi wake wa kutusumbua wananchi wenzie!
Hata mawazo yakufikiria na kuplan hii migomo,mgao wa umeme n.k tunashindwa !
Nlitaka niende kwa mwenyekiti wa SM ni sawa?
Kama kuna wajuzi zaidi nsaidieni.
Nawakilisha kama nawewe uliwahi kuipata kero hii iweke humu.
 
kamwone mwanasheria akushauri jinsi ya kufungua kesi mahakamani, maana kuna sheria ya nuisanse katika 'tot laws' za kumbana huyo jirani yako
 
Pole sana.
Endapo, Sheria ya nchi na sheria ndogo ya Halmashauri ya Mji wako inayohusu utulivu, kutowasumbua jamii na pia kutochafua mazingira (air pollution) zikishindwa kumtia hatiani, basi wakati wa kwenda likizo au safari fulani, wewe tafuta kijana akae hapo kwako na umpe muziki mnene wa Disco kama wa dB Drag Racing na ahakikishe kuwa anamfungulia full blast tena acheze zile miziki ambazo huyo jirani yako hazipendi hususani za kufoka utapata majibu ukitoka likizo!
 
tafuta pikipiki(tukutuku) chomoa bomba ya moshi. Piga piga race nawewe asubh,mchana na usiku...majirani wenzio watalalamika hapo ndipo uwakumbushe na hiyo adha yakwako! Usijali gharama ya petrol.
 
kamwone mwanasheria akushauri jinsi ya kufungua kesi mahakamani, maana kuna sheria ya nuisanse katika 'tot laws' za kumbana huyo jirani yako
Jaman nlivyomuelewa huyu mwenzetu anahitaji masaada wetu...hili la kwenda amuone lawyer nahisi litamuongeza gharama zisizofaa juu yake!
Sijaupuuza ushauri wako.
 
Naskia unaruhusiwa kumtumia barua ya ya warning and intention to sue

unampa wiki tatu ajirekebishe asipojirekebisha mpeleke mahakamani

Mi nilimtumia jirani yangu hiyo barua in 2009 at that time nilikua nafanya mitihani alafu yeye anasumbua usiku

In two days time alikua anazima mziki wake sa tatu usiku au anaweka sauti ya chini

Try that trick, pengine hajui kama anavunja sheria

kikatiba hairuhusiwi mtu kufanya starehe kwa kuwakwaza wengine
 
Hiyo ni public/private nuisance. Wazo la kuanzia kwa mwenyekiti SM ni zuri kabla kumshitaki on private/public nuisance!
 
Pole sana - yaani mitaani kuna KERO nyingi sana -

Wewe unalalamika SAUTI KUBWA YA RADIO - wengine MAJIRANI WANAFUGA NG'OMBE/KUKU/NGURUWE............harufu inasambaa mtaa mzima - halafu samadi inawekwa mbele ya nyumba ambapo ni barabara - hivyo unapopita ni uchafu mtupu - era hii ya 2011
NCHI YA TANZANIA NI KERO TU - UFISADI, UCHAFU..........

unaweza kumshitaki lakini suppose akaanza uhasama na wewe??? mwite kikao uongee naye umwelimishe somo la USTAARABU labda halijui
na naamini ataelimika ........... asipokusikia ..........hapo tena - chukua hatua ingine ya kisheria.
 
hyo kaa nae chine mweleeze anavyokukera kwa kufungulia radio juu akikataa tafuta pikipki toboa mafla elekeza dirishani kwake piga resi weee nakwambia atakuja kuomba samahani mwenywe
 
Pole sana - yaani mitaani kuna KERO nyingi sana -

Wewe unalalamika SAUTI KUBWA YA RADIO - wengine MAJIRANI WANAFUGA NG'OMBE/KUKU/NGURUWE............harufu inasambaa mtaa mzima - halafu samadi inawekwa mbele ya nyumba ambapo ni barabara - hivyo unapopita ni uchafu mtupu - era hii ya 2011
NCHI YA TANZANIA NI KERO TU - UFISADI, UCHAFU..........

unaweza kumshitaki lakini suppose akaanza uhasama na wewe??? mwite kikao uongee naye umwelimishe somo la USTAARABU labda halijui
na naamini ataelimika ........... asipokusikia ..........hapo tena - chukua hatua ingine ya kisheria.
Mhhhh!
Tz !!!!!!!!hiyo
 
Kaka kwenye maelezo yako sijaona kuwa umefanya jitihada zozote za kimazungumzo, zikashindikana ndio ukaja JF. Hebu jaribu hilo kwanza, wakati mwingine hatua zinazoweza kuleta uhasama si nzuri sana kufuata!
 
mwone afisa afya wa mtaa wako kwenye bkila kata kuna afisa afya,mwende pamoja na hakikisha

mwone afisa afya wa mtaa wako mkiwa na mwenyekiti wa SM mkamateni na mfikisheni mahakama ya jiji pale mtawakuta waendesha mashtaka Kijumbe(Kinondoni) au MUnga(Ilala)Hiza (temeke) wataaandika hati ya mashtaka na kumfungulia kesi.fanya fasta usitoe chochote kwa maafisa afya manake ndio zao na usikublai wamwachie manake watadai hongo kwake mziki utaendelea.ukishindwa ingia chemba hapa JF ntafute nikupe njia mbadala.
 
Back
Top Bottom