LIKUD
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 19,349
- 36,303
Dalili zote zinaonyesha kuwa uwezekano wa Tanzania kuvuka mwaka 2015 bila kutokea machafuko ya nchi nzima kati ya wakristo na waislamu ni mdogo sana. Sidhani kama napaswa kulielezea sana suala hili hapa JF. Kuna kundi la wapuuzi fulani hivi hapa Tanzania, wanataka kufanya majaribio ya vita vya udini.Mimi ni Mkristo Mkatoliki, nimelelewa katika misingi ya kikristo. Tabia kuu ya wakristo popote duniani ni kupenda amani. Siwezi kuishi katika nchi isiyokuwa na amani. Vita hivi vikitokea ( SIOMBEI IWE HIVYO ) vinaweza kudumu kwa mwaka mmoja hadi mitatu ( KAMA ITAKUWA BAHATI YETU ) au kudumu kwa Muongo mzima ( GOD FORBID ). Kufuatia hali hiyo basi, ninajiandaa kuikimbia nchi hii kabla ya mwezi Juni 2014 ( kama nitajaaliwa uhai ) (Ingawa inaniuma sana kufikiria kuimbia nchi ninayo ipenda kuliko chochote )..Nimepanga kwenda kuishi katika visiwa vya ST.Lucia, ama Barbados, ama Bahamas ama Jamaica. Uwezo huo ninao, vipi kuhusu wewe mwenzangu na mimi wa Manzese unaye shabikia udini, machafuko yakitokea utakimbilia wapi weye kama sio Kisarawe ama Rufiji ambako nako kutakuwa na macahafuko? Acheni upuuzi wenu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA, AMEEN!
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA, AMEEN!