Maoni, Mawazo & Ushauri kuhusu biashara ya Rasta na Weaving

MAKA PEN

Member
Feb 23, 2015
20
6
Wadau habari.

Kwa mtu yeyote yule anaifahamu vizuri biashara ya nywele zinazotoka nchini China naomba anifahamishe, sina uelewa kabisa na hii biashara. Ningependa niifahamu vizuri nione kama inafaa au la.

Nimepata supplier mmoja kutoka China, amesema wao wanauza kwa kilo. Ambapo nusu kilo wanauza 35 USD, kwahiyo sijafahamu ukija nchini unauzaje ni kwamba unazipunguza toka nusu kilo na kutenga kidogo kidogo na kuanza kuuza.

Endapo nikaamua kuchukua nusu kilo kwa dollar 35, je unadhani naweza kupata faida ukijumlisha gharama za kusafirisha pamoja na ushuru wa TRA.

Karibuni sana wadau tujadiliane ili tujue ni namna gani tunaweza kujiongezea kipato.

============================================

Biashara ya saluni inalipa sana. Mfano dazeni ya nywele za bandia ni sh.12000 tu (kwa bei ya jumla jumla) ambapo kwa reja reja kila pic moja inauzwa sh.1600 tu.

Hivyo ukiwa na dazeni 100 na kila dazeni ina pic 12 ili itimie dazeni, hivyo,

Kila pic moja kama utaiuza sh.1600 utapata faida ya sh.19,200 (yaani 12 zidisha kwa sh.1600)

Hivyo, chukua faida ya dazeni moja ambayo ni sh. 19,200 zidisha kwa dazeni 100 utapata sh.1,920,000. Hata ukifanikiwa kumaliza hizo dazeni ndani ya mda mfupi hiyo hela itakuwa yako yaani faida.

KUMBUKA: Hapo unahitaji mtaji wa sh.1,200,000 tu. Pia biashara hii hakikisha huna Tabia za kutamani tamani wanawake maana faida hutaiona!

Kazi ni kwenu sasa!
 
kwa ambaye pia anajua brand nzuri ya nywele na style zake naomba aniambie wadau
 
Ni kama huna abc's za biashara yenyewe, si ungepita hata kwenye maduka ukaangalia wauzaji wa rejareja wanauza kwa ujazo gani, au uliza wenye saluni au hata kinamama/dada wa kitaa na ujionee sampo wewe mwenyewe ujiridhishe kabla hujaamua.
 
Wadau habari.

Kwa mtu yeyote yule anaifahamu vizuri biashara ya nywele zinazotoka nchini China naomba anifahamishe, sina uelewa kabisa na hii biashara. Ningependa niifahamu vizuri nione kama inafaa au la.

Nimepata supplier mmoja kutoka China, amesema wao wanauza kwa kilo. Ambapo nusu kilo wanauza 35 USD, kwahiyo sijafahamu ukija nchini unauzaje ni kwamba unazipunguza toka nusu kilo na kutenga kidogo kidogo na kuanza kuuza.

Endapo nikaamua kuchukua nusu kilo kwa dollar 35, je unadhani naweza kupata faida ukijumlisha gharama za kusafirisha pamoja na ushuru wa TRA.

Karibuni sana wadau tujadiliane ili tujue ni namna gani tunaweza kujiongezea kipato.

nywele? any way goodlucky buddy!
 
Ujinga wa waafrika. Unanunua nywele za bandia wakati unazo nywele. Inferiority complex. Kipilipili ndio nywele za kiafrika. Ni kituko uko mweusi tii halafu nywele blond. Unaonekana kituko.
 
Hapo inategemea kama kweli ni original human hair, na pia ujue kama ni virgin au remmy human hair, pia ufanyie biashara jiji kama la dar ambalo watu wanajua weaving original na wanafika bei, weaving feki zinaua sana soko. Kuhusu usafirishaji na ushuru sina uzoefu hata kidogo. Pia ujue kama wameshazitreat kwa ubora unaotakiwa.
 
Japo mi si mtoa maada hata mimi pia nipo kwenye mchakato wa kuagiza nywele toka china, muuzaji anauza original human hair, virgin and unprocesses kwa USD 34/0.5 kg ambapo 0.5 kg inaweza kutumika kwa watu wanne. Kwahiyo 0.5 kg ni sawa na 61,200 kwa pesa ya Tz ambapo ukigawa kwa watu wanne ni sawa na kununua nywele za kumtosha mtu mmoja kwa sh 15,300 pamoja na usafirishaji na kila kitu haitazidi elfu 30. Je, hapa Dar nywele bundle moja zenye sifa tajwa hapo juu zinauzwaje? unaushari wowote kuhusiana na nilichoandika hapo juu.
Asante na Karibu ladyfocus
 
Last edited by a moderator:
Mfano mtu ana mtaji 2M Tshs, anataka afungue duka la RASTA na WIVING.... anapenda kujua ni rasta na wiving za aina gani ambazo ni nzuri na quality na zipo kwenye trendd?
pia anauliza wapi hapa dar es salaam anaweza kupata mzigo wa jumla kwa bei rahisi?
 
Kuhusu kujua ni aina gani nzuri za weaving jaribu kuongea na kina dada pamoja na kina mama ambao ndo wateja wakubwa ili waweze kukuambia ni zipi zenyr soko zaidi
Kuhusu upatikanaji wa mzigo hiyo simple we jipeleke kkoo kuna mtaa wenye maduka ya bidhaa hzo pekee
 
Wadau mimi nataka kuanza kufanya biashara za mawigi, rasta na weaving mwenye utaalamu na hii biashara naomba updates nataka nifanyie huku mikoa ya nnyanda za juu kusini.
 
Waungwana,

Natafuta hizo nywele kwa bei ya jumla na wapi zinapatikana kwa viwango gani mwenye nazo please anisaidie ubora wake.

Ahsanteni
 
Back
Top Bottom