Nataka kuacha kazi/kuajiriwa ili nijiajiri

Kwanza usiache kazi, pili biashara ya mchele/mpunga inapasua kichwa kidogo ni bora ufanye utafit na uangalie masoko. Lakini yapo mazao mengine ambayo yanalipa na mara nyingi wengi wanayapa kisogo, kama tangawiz, swaumu, kitunguu maji, maharage lakini pia yanategemea na soko na msimu. so u better utafiti before u dive in. Mazao mengne ambayo si mshauri mtu yeyote afanye ni Nyanya, Matikiti, Hoho etc sababu ni perishable na soko lake linalazimishwa na demand au expiry time ya bidhaa yenyew.
All the best Kaka.
 
Hili wazo la kuacha kazi na kujiajiri ni wazo limekuwa likitusumbua waajiriwa wengi ila nazani udhubutu ndio haswa linalotuponza tulio wengi
 
3.5 laki au tsh?
Kama kweli huyu jamaa ni tajiri mkubwa,kasema 3.5 million ila yeye ameandika 3.5 millions. Pesa yote hiyo si unafanya kila unachokitaka na unawekeza.Kama ni kweli basi kuna tatizo mahli katika mifumo na akili zetu.Sipendi ujinga.
 
Kama moyo wako unakutuma kuacha kazi basi acha,ila usiache ili uende kulima...kilimo cha bongo kitakufirisi utajuta maisha yako yote.

Anza na biashara ya kuiona hela daily, then utalima ukiwa na misingi.
Mawazo mazuri kama haya ingebidi tuwe tunalipia,,,,asante mkuu, nmepata cha kujifunza toka kwako
 
kama kweli umeamua toka moyo.. narudia tena toka moyoni na uko radhi kuface challenges ahead acha kazi. Mimi nilikua nafanya kazi katika mgodi flani na nilikua nalipwa 16.5M na ilinichukua miaka mingi kufikia uamuz wa kwako wa kuacha kazi ila mwishon nilifanikiwa nikaanza na biashara na Nashukuru Mungu mambo co mabaya ila usitarajie mafanikio ya haraka maana kuna kipindi hata ile pesa niliyokua naipata kama mshahara nilikua naitaman so usivunjike moyo na KARIBU kwenye Ujasiriamali.
Daaah.,,,mkuu,,,unamaanisha 16.5 milion taslimu?????,,,,ama kweli njaa sio ya wote
 
Kwanza napenda kukupongeza kwa kuajiriwa, pili kunmbuka si lazima kukimbilia kuacha kazi, jaribu kuitumia hiyo ajira kama dhamana kupata mikopo ili uweze kufanya mambo yako mengine.

Kwenda kulima ni vema ila kabla ya kuingia huko jaribu kupata ushauri kutoka kwa watu ambao wana uzoefu wa kilimo ili wakueleze faida na changamoto wanazokumbana nazo ili ukiingia huko uwe umejipanga jinsi ya kupambana, maana nasikia huko kwenye kilimo kuna shida sana ya vibarua unaweza wewe ukawa chanzo tu cha kuwapatia hao vibarua ajira na wewe ukaishia kuondoka mikono mitupu!

Nina jamaa zangu kibao ambao walijiingiza kichwakichwa almanusura wawe vichaa kwa hasara waliyokutana nayo.
Mimi binafsi sishaur mtu kuajirwa na fanya biashara kwani hao watu utakaowaachia hiyo biashara yako hawana uchungu wowote na hela yako kwan hawajui shiling ngap ni faida na ngap ni hasara trust me utafunga hata kabla ya mwaka kupita. Nmepata hasara ya zaidi ya 14 mil kutokana na hilo wazo la kukomaa kwanza kwenye ajira then hela niweke kwenye biashara. Fikiria Bill Gates angeajirwa microsoft inhekuwepo. Kikubwa usiwe na hofu na maamuzi yako yaamin kwanza maamuzi yako plus kabla ya kutoka hakikisha kwanza familia yako umewajenga kisaikolojia kwa hilo unalitaka kufanya kwani mnaweza kupitia kipindi kigumu lakin wawetayari kwa lolote ni muwetayar kufarijiana na sio kulaumiana kwamba baba unaona sasa hatuwez hata kula nyama mwez mzma. Na ugumu ni kipind cha mwanzo tu. Kkubwa kuwa na connction na taarifa sahihi kuhusu unachotaka kufanyathen hapo fanyamaamuzi magumu. Mm nilianza kujianda kuachakazi the first day naenda kuripoti kazi baada ya mwez nilianda barua ipo inasubiri siku yake. Kuna jamaa nafikiri ni chasha yeye anasema unachoma meli.
 
Wakuu;

Niko katika ajira mwaka wa nne sasa tangu nimalize shule. Gross Pay yangu ni 3.5 milioni plus. Lakini nikiangalia mbele i dont see my self being rich kwa kuendelea na maisha haya ya kuajiriwa.

Naweza Ku-raise 10Millions kama mtaji wa mwanzo ili kuondoka kwenye Ajira. Natazama maeneo mawili ya kujiajiri;

1.Kufungua Professional Firm (Partneship) itakayotoa Law services, Consultancy, Auditing and Accounting services. Ofisi zake ziwe nje ya mji.

2. Kwenda kukodi mashamba takribani hekari 30 Morogoro nilime Mpunga full time.

Naombeni mnipe Ushauri kuhusu Calculations zangu hizi.

cc Koba Ogah Mzuzu Chipukizi Pasco Patriote Asante ssalaf MeinKempf Malila dolevaby Chiwa busiminet muvimba Ukweli1 Elinanho
Mkuu mimi niko katika ajira kama wewe ila kwa mshahara chini ya wako, na nimekuwa nafanya kazi na huku najishughulisha na kilimo & ufugaji kwa zaidi ya miaka 20 sasa. Kujiajiri kwa kutegemea kilimo tu kunahitaji kujiandaa kwa mambo mengi baadhi ni kama yafuatayo;-
1. inabidi uwe na shamba lako mwenyewe
2. inabidi uwe na namna ya kupata maji mwaka mzima
3. ujue aina mazao utakayoenda kulima changamoto zake na masoko yaliko.
4.Uwe na mtaji wa kutosha kwa ajili ya pembejeo
5. uwe na mtaji wa ziada( redemption money) tambua unaweza kulima ukavuna chini ya malengo au usivune kabisa
6.shamba lako liwe karibu na masoko if possible and reliable way of transport iwepo mpaka shambani au karibu na shamba.
7.uwe na task force ya watu waaminifu na wenye bidii pia wasiwe wapenzi sana wa kinywaji kikali.
8.Shamba usimamie mwenyewe au mtu wa kuaminika ( hapa ndo pana kazi)
9.Mengine wataongezea wenzangu, mimi ninayo mashamba Morogoro mikese ma Dodoma vijiji mbalimbali. Nakushauri usiache kazi kabla ya kujaribu mradi unaotaka kuufanya na matokeo yake ( rafiki zangu wengi walioacha kazi au kuchukua mikopo walijuta sana na wengine kupoteza maisha kwa kuingia wazima wazima na baadae mambo kuwaendea ndivyo sivyo.
Nakushauri kama uko Dar au maeneo ya Morogoro nitakuazima shamba ekari tano au kumi bure ufanye majaribio kwanza huku ukijizatiti kama nilivyokushauli.
 
Back
Top Bottom