Kaka Escober ebu tusaidiane kidogo,watu wengi wenye hiace utupia lawama zao kwa madereva pindi wanapopewa matatizo ya gari zao,sijui unataka kwa matumizi gani lakini kianzio cha bajeti yako kwa super roof manual ambalo ni Diesel 8ml ni kidogo sana,ata uagize nje ya nchi hiyo 8ml ni bei ya ushuru kwa super roof isiyo na dumping fee.Fanya hivi kama unataka kwa ajiri ya daladala nunua gari nzuri si bora hiace.Nilinunua hiace super roof manual disel ya 2004 Dubai,kwa $7500 ushuru ni 8ml lakini tangu niiweka njiani mwaka juzi 2012 kila siku dereva analeta tsh 60000 bila kuaribika wala nini,nafanya service ndogondogo tu..kuna watu wanasema biashara ya hiace ni pasua kichwa,kwa uzoefu wangu mdogo naelewa si pasua kichwa ila watu wananunua hiace cheap wakitegemea kupata faida kumbe ni matatizo matupu,ata mtu akikuuzia super roof Diesel manual kwa $10000 mchukue fundi kwanza na kuliangalia hilo gari...Automatic ambayo ni Petrol ni cheaper lakini si mazuri kwa biashara