Natafuta sehemu ya kufanya field work

ubma

Member
May 24, 2016
28
7
Habari Members wa jamii forum,

Tafadhali naomba husika na kichwa cha habari hapo juu.

Mimi ni kijana wa kiume na ni mwanafunzi wa chuo cha Cha elimu ya biashara CBE ngazi ya (Diploma in Business Administration) mwaka wa kwanza, ninakuja mbele yenu kuomba msaada kwa yeyote mwenye kuweza kunisaidia kupata sehemu ya kufanya field kwa muda wa mwezi moja, nimehangaika kutafuta sehemu nyingi Sana lakini sikuweza kupata na ukizingatia muda wa kuanza field uliowekwa na chuo kwa mujibu barua ambayo inatutambulisha umekaribia kuisha na kila sehemu niliyoenda naambiwa acha barua na tutatoa list mwezi wa 6.

Nimekaa nikatafakari nikaona ni bora nije kuomba msaada kwa wanaJamii Forum labda mnaweza kunisaidia, na sihitaji kulipwa maana kuna sehemu ninafanya kibarua hivyo nitachukua likizo ili nifanye field maana nilijaribu kuomba field sehemu ninayofanyia kazi nikakutana na urasimu mkubwa hasa baada ya wahusika kugundua kuwa ninasoma Ndipo vikwazo vikaanza mpaka mahudhurio yangu ya chuo yakawa hafifu ila ninaendelea na masomo kama kawaida kwa uwezo wa Mungu.

Hivyo naomba wana Jamii forum kwa yoyote mwenye kampuni au taasisi ambayo anaweza kunipatia Fursa ya kufanya field nipo tayari kuleta barua yangu ya utambulisho toka chuo na hata kama atahitaji vielelezo vingine nipo tayari kuviwasilisha ili nipate acceptance letter ambayo nitaiwasilisha chuo ili wanipangie Lecture atakayekuja kunikagua na kuendelea na field, Nawasilisha .
Ahsante.
 
Mungu akubariki saana. Haya mambo yanasumbua kwa baadhi ya kozi....
Jaribu kwenda kwenye makampuni yasiyo na umaaruf saana ambayo watu wengi wanayagombea...

All the best
 
Mungu akubariki saana. Haya mambo yanasumbua kwa baadhi ya kozi....
Jaribu kwenda kwenye makampuni yasiyo na umaaruf saana ambayo watu wengi wanayagombea...

All the best
Ahsante Sana mkuu kwa kunitia moyo, ngoja niendelee kuitafuta.
 
Mungu akubariki saana. Haya mambo yanasumbua kwa baadhi ya kozi....
Jaribu kwenda kwenye makampuni yasiyo na umaaruf saana ambayo watu wengi wanayagombea...

All the best
Mfano wa hizo kampuni ambazo sio maarufu???
 
Back
Top Bottom