Natafuta rafiki wa kike

Feb 15, 2013
55
125
Naitwa smart introvert, nakuja mbele zenu kutafuta rafiki wa kike ambae tutabadilishana mawazo na kujenga urafiki mzuri. Umri wangu miaka 28 na nafanya kazi kampuni moja. Naishi Dar na ni mkristo.

Naomba rafiki awe wa kike,mpenda maendeleo,angalau awe na elimu ya diploma, dini zote ila mkristu ni vizuri zaidi, awe mtu anaependa kujifunza, awe na miaka 19 hadi 30 na pia anaishi Dar.

Karibuni sana inbox tupate kufahamiana
 

Zabron Hamis

Verified Member
Dec 19, 2016
3,383
2,000
Hamna urafiki kati ya mwanaume na mwanamke..sema tu unatafuta wakukusaidia kula mshahara wako
Hahahahaaaa!!!! Labda kuna ukweli ndani yake. Lakini kuna baadhi ya watu wanaweza kuwa hv. Na huishi kwa furaha sana pengine kuzidi hata wapenzi. Uzuri wa kuwa na rafiki wa jinsia tofauti na yako unapata elimu na ukimpata anayekuheshimu na kukupenda kama nduguye, matatizo utayasikia kwa jirani. Tatizo ni pale utakapompata rafiki asiyekujali, utaishia kuumia na kujilaumu kwann ulikutana naye. Binafsi ninaye rafiki na nilikutana naye humu jf, bahati mbaya tumepotezana kwasababu ambazo siwezi kuziweka hapa, ila kwa muda tuliokuwa pamoja niliinjoi sana na ni mwanamke aliyekuwa akinitia moyo, alikuwa akihakikisha nimelala au tumeagana ndipo nayeye alale. alaaniwe shetani aliyetupoteza maana ndio kwanza urafiki ulikuwa umenoga. I wish bado awe yupo humu jf asome ujumbe huu aje inbox. I miss you very much my younger sister. Hope one day we shall meet either on earth or in heaven (uwezekano wa kwenda motoni ni mdogo sana). Nakumbuka siku tuliyoongea mpaka saa tisa usiku, kulipokucha asubuhi tulikuwa na usingizi lakini ulihakikisha umenijulia hali nduguyo. Kama ukiona ujumbe wangu, usiache kunitafuta maana nimekukumbuka sana.

Naomba niishie hapa maana nimekumbuka mbali sana. Niko njiani kuelekea dodoma
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom