Dada tangu naanza JF leo kwa mara ya kwanza nimekutana na hitaji la kipekee.....Hivi yule mdogo wetu aliyekataa shule darasa la 4 una taarifa zake maana tusipomshtulia hii fursa atakua mzigo kwetu baadae.hivi kumbe ni mmu nkajua nipo jukwaa la nafasi za kazi na tenda
Ukereketwa wa haki sawa maana yake ni nini? vigezo vingine navi meet ila hiyo sijaelewa mchumba mtarajiwa?
aisee....uishie chekechea na uwe mpenda maendeleo...seems weird...
Mbona kawaida tu....nna watu kibao mi nawajua kusoma wamejulia ukubwani ila ni wanasaka pesa na wamefanikiwa hadi kero
Hizi si sifa za mke hizi sifa ni za.mfanyakazi sijui kama ni wa ndani!!!!!!!
Rejea kichwa cha habari.
Nina umri wa miaka 29, elimu yangu ni chuo kikuu.zifuatazo ni baadhi sifa muhimu za mke naemuitaji :
1.Awe mcha Mungu ( mkristo )
2. Awe mwenye maadili ya kiafrika.
3.Awe na elimu yoyote hata kama aliishia chekechea
4.Awe mpenda maendeleo ( asiridhike tu na uhakika wa kupata chai asubui na chakula)
5. Sio lazima awe na kaz kwa sasa, awe nayo asiwe nayo sawa.hata kama amejiajiri sawa.
6.kabila lolote na rangi si muhimu
7. Asiwe mwemba, umbo la wastan
8.kama ana mtoto bahat mbaya,bas asizid mmoja kwan naamin mmoja hatanisumbua sana ktk malez
9. Umri wake kuanzia 18- 26
10. Urefu wake uwe wastan tu au zaid.
11. Asiwe mkereketwa wa haki sawa
12. Mvumillivu, mwaminifu, msiri wa mambo ya ndani.
13. Asiwe mjuaji kupitiliza (much know) , yan akubali kujifunza kutoka kwa wengine pale inapotokea kakosea.
14. Ajue wajibu wake kama mke
Hayo ni mambo ya msingi sana kwangu, nipo serious naomba sana tuweke pembeni utani ,kashfa na kejeli, kama hauna kizur cha kupost ni jambo jema kukukaa kimya waheshimiwa. Mwenye uhitaji kama wangu tuwasiliane kwa private message (PM). Yes
..unaifahamu elimu ya chekechekea lakini mpaka iwe kawaida.....
..kwenye red..wa ngapi kati ya wangapi mpaka iwe ni ''kawaida''
Dada tangu naanza JF leo kwa mara ya kwanza nimekutana na hitaji la kipekee.....Hivi yule mdogo wetu aliyekataa shule darasa la 4 una taarifa zake maana tusipomshtulia hii fursa atakua mzigo kwetu baadae.[/QUOTE
Mbona watu mnashangaa hivyo sana jamani, inaonekana haijawai tokea toka dunia kuumbwa nn? . Naona kwenye elimu ya chekechea hapo ndo watu wengi wanashangaa hasa kwa graduate kuandika kuwa hata chekechea ruksa, mwenzenu sioi elimu ya mtu bali naoa mtu bas, ndo mana elimu sio kipaumbele sana kwangu.hiv katika biblia mke wa adamu alikuwa na elimu? Narudia tena hivyo ndo vigezo vyangu na mm ndio ntakaeishinaye sio mtu mwingine
Dada tangu naanza JF leo kwa mara ya kwanza nimekutana na hitaji la kipekee.....Hivi yule mdogo wetu aliyekataa shule darasa la 4 una taarifa zake maana tusipomshtulia hii fursa atakua mzigo kwetu baadae.
Elimu ya chekechea si yule ambaye hajaingia shule ya msingi....kuhusu hao watu mi sijawahi kuwafanyia sensa nikajua ni ngapi kwa ngapi
...uchache wao/wingi wao ndio itaonesha kama ni kawaida ama la...
Ninaowajua mimi ni wengi
...haibadilishi ukweli si kawaida...elimu ya msingi ni basic(foundation level)......a compulsory(unajua kwa nini)...
Huo ukereketwa wa haki sawa mimi hoi
Jf never boreng