NATENGENEZA KIZAZI CHA WANAUME NA SIO WAKIUME.
Huoi ili upikiwe na ufuliwe nguo, kupigiwa pasi na kutandikiwa kitanda, maana hata house girl anaweza kufanya yote hayo. Pia huoi ili tu utimiziwe haja za kingono, kusema kweli wengi mnapata hizo huduma hata bila kuoa. Tusiigize hapa.
Kama kula unakula hotelini, American Chips na maeneo mengine mengi. So hilo sio hitaji serious. Sasa unaoa ili iweje kama yote hayo unaweza kuyapata bila mke?
Mwanamke ameitwa kuwa msaidizi na sio kijakazi. Maana kama unaoa ili kupatiwa mahitaji ya nyumbani (domestic chores) basi huyo ni mjakazi. Na mjakazi au kifupi mtumwa anamipaka. Huwezi kumruhusu akakujua sana kwani hajavuka level ya utumwa na kuwa rafiki.
Mke kama msaidizi anapaswa kuhusika na maisha yako kwa asilimia 100%, na sio 50%. Lazima upate mtu ambaye umemkagua na kuridhika naye kwamba anauwezo na kifua cha kubebana na ndoto zako. Zaidi sana awe ni mtu unayempenda kutoka ndani. Kwa kusema hayo namaanisha huwezi kuoa kwa kushauriwa na rafiki zako eti "Huyo mnaendana Sana?"
Oga! Hata Mungu anamuuliza Yeremia "Unaona nini?" ni jukumu lako kusema kile unachoona na sio watu wanachokuambia.
Bro, NDOA sio suti kusema ikikubana unagawa na kununua nyingine, la hasha. Hupaswi kuingia kichwa kichwa bila kujua hata sababu kwa nini unataka kuoa.
Ukweli kwamba rafiki zako wote wana wake zao bado sio sababu ya kutafutia mke. Ukweli kwamba wazazi wanatamani mjukuu bado sio sababu tosha ya kuingia kwenye Ndoa. Ukweli kwamba Maaskofu wako wanataka wakupe uchungaji pia bado sio sababu ya kutafutia mke.
Mke ni msaidizi, sasa wewe una nini cha kusaidiwa? Mke anakuja kukukamilisha, hapo lazima uwe umejitambua kusudi la kuumbwa kwako ili upate mtu mwenye uwezo wa kuungana na wewe kukusaidia kulitimiza. Sasa kama wewe mwenyewe hajuelewi mpaka sasa bado unaona ni fahari kugalagaza wanawake tofauti-tofauti kitandani kwako. Bado unaona ni ujanja kuchanganya wanawake, bado unajisikia fahari kupiganisha mabinti, wewe hauko tayari kuoa.
Biblia inasema "Kwa hiyo Mwanaume atamuacha Baba yake na Mama yake naye ataambatana na MKEWE...." (Mwanzo 2:24) Ndoa ni kwaajili ya Wanaume sio WAVULANA, hayo mambo unayofanya ni ya Kivulana. Hata kama ndevu zimeanza kutoka mvi unaweza kuwa mvulana bado kwenye ufahamu. So unahitaji kukua. Na NDOA haikusaidii kuacha uasherati ila unaamua kuacha uasherati ndio unaingia kwenye Ndoa.
Usikimbilie kwenye Ndoa kama kuna vitu hujaweka sawa maana utaenda kuwa mzigo kwa mtoto wa watu.
Kama hujaweza kufanya maamuzi ya maisha yako na kuyasimamia, bado hadi hela ya nguo unapewa na wazazi wako, wewe hauko tayari kuoa, maana hata ukioa maamuzi ya chumbani kwako yatafanywa na wazazi wako na utampa shida mwenzi wako.
Hebu anza kwanza kujifunza kuwa mwanaume, kuwa kichwa na kiongozi. Kama huwezi kuongoza hicho kichwa katikati ya mapaja yako, sidhani kama unaweza kuongoza kichwa cha mke na watoto wako.
Unawezaje kujiita mwanaume na wakati huwezi hata kulinda hisia za Mtu unayedai kuwa unampenda?
Dah usiseme nimewaamulia ila natakakuwasaidia.
Kusimamia harusi ikafanyika ni tofauti sana na kusimamia NDOA yako. Bro, harusi inakuwaga na kamati. Na unaweza ku-deligate majukumu na ukasaidiwa. Ila kwenye Ndoa unapambana mwenyewe. So kuwa mwanaume kwanza kabla hujaruka hatua na kukimbilia kuwa Mume. Anza kujiongoza na kujisimamia kabla hujataka kuongoza nyumba yako na watoto wako. Kwa Leo naishi hapa. Ukitaka maandalizi haya jiunge na BAM SOCIETY pahala WANAUME WANATENGENEZWA.
#UANAUME_NI_MAJUKUMU.
-Pastor Nick Shaboka Jr
New Day Church Tanzania
+255715310587