Ndugu wana JF, natumai hamjambo!
Naomba mnisaidie wapi naweza kupata miti ya matunda yafuatayo? Nahitaji angalau miti miwili katika kila aina.
Nahitaji mnisaidie kunielekeza nitakapozipata, contacts na if possible na bei zake:
(1)Zabibu (nyeusi na za kijani) - jumla miti minne
Ukipata mtu kutoka Dodoma unaweza kuzipata. Ila zile seedless za kijani sidhani kama unaweza kuzipata hapa Tz
(2)Strawberry - miti miwili
Sidhani kama unaweza kuotesha strawberries Mtwara, ila nimeona zinauzwa Morogoro huwa zinatoka kule milimani juu ambako kuna baridi sana
(3)Zeituni - miti miwili
Unataka zeituni ipi, olives au ile yenye matunda ya manjano inayoitwa "Shajarati Fatma" kwa Zanzibar? Ikiwa ni hiyo ya pili basi ni rahisi kuatika mbegu na iko mingi katika maeneo ya pwani kama Tanga. Ama kwa olives huwa zinaota kwenye sehemu ya baridi na hasa maeneo ya Mediterranean sidhani kama unaweza kupata miti yake hapa Dar
(4)Dates (tende) - miti miwili
Chukua mbegu za tende mbili na uoteshe ni rahisi sana. Ukiona haioti jaribu kukwangua lile gamba la juu kwani baadhi ya mbegu hasa zile zenye gamba la nje gumu hulazimu kulikwangua au kuchemsha ili kuruhusu mche utoke.
(5)Apples (tufaa) - miti miwili
(6)Pears - miti miwili
Hii inahitaji baridi ili iweze kuzaa matunda. Miche yake utapata maeneo ya Iringa (Mufindi huko) au Lushoto Tanga
(7)Pomegranate (komamanga) - miti miwili
Hii unaweza kupata kwenye nursery za binafsi, au umuombe mwenye mti huo binafsi akuoteshee
(8)Mulberry (forosadi) - miti miwili
Hii miti ya porini kwa kwetu lakini unaweza kupata kwa watu binafsi
(9)Tangarine (chenza) - miti miwili
Michenza unaweza kupata kwenye nurseries nyingi lakini angalia unataka ya aina gani, ya mbegu au ambayo imefanyiwa budding? Ni vyema ukapata michenza ambayo imefanyiwa budding, yaani rootstock (kigogo) ni cha mlimau halafu imepandishiwa michenza. Hivyo utapata miche itayokuwa na ustahmilivu zaidi wa maradhi mbali mbali ya citrus.
(10)Na miti ya matunda mengine mengi kadiri mtakavyoona yatanifaa, sana sana mimea inayostawi sehemu ya joto - nataka niipande Mtwara.
Nitashukuru.