Hapana Mkuu. Huzaliwa na mkia but huwa inakatwa kwa mapenzi ya mfugaji. Nowadays binafsi napenda abaki na mkia.
Kukatwa kwa mikia kuna sababu zake pia, ikiwemo asili ya huyu mbwa, security wise na matamanio ya mfugaji.
Asili ya Rottweiler walikuwa wanatumika kwenye mashamba kuburuta mizigo na hivyo ilionekana akiwa na mkia unamtinga kufanya hiyo kazi ipasavyo the wakaanza hiyo kukata mikia. Lakini pia iliaminika kwamba ukikata mkia, mbwa huwa na afya zaidi.
Security-wise; mbwa asiye na mkia ni ngumu sana kujua kama amefurahia uwepo wako au lah. Mara nyingi mbwa akifurahia uwepo hisia ya kwanza huwa kwenye mkia kwa kuuchezesha. Sasa asipokuwa na mkia ni ngumu kumjua.
Na upande wa matamanio ya mfugaji ni kama vile wengine u-crop masikio ya mbwa kama Doberman.
Sababu ingine ya kukata ni kwa sababu mikia yao huwa haiendani na miili yao kwa kuwa miembamba.
Machache ni hayo.