Natafuta Kazi

Natafuta Kazi

Joined
Aug 17, 2021
Posts
6
Reaction score
6
Habari wakuu,

Naitwa Khalifa Nassoro ninaishi Kitunda-Banana, Dar es salaam. Nimesoma Bachelors degree in Accounting and Finance (BAF) chuo kikuu Mzumbe, Morogoro 2021.

Nina umri wa miaka 25. Nilivyomalizaga chuo niliamua kubaki Morogoro katika miangaiko ya hapa na hapa nikapata ofisi ya kutoa Mikopo nikafanya kwa takriban miezi 10 kama Afisa Mikopo (Loan Officer) nikashindwa kuendelea maana maisha yalikuwa yananishinda pale kwakuwa hatukuwa tunapewa chochote zaidi ya kufanya ujanja ujanja upate chochote kitu uweze kuishi.

Ombi langu kuu kwenu ni kuomba fursa kwa anayeweza nisaidia niweze kupata kama ni sehemu ya kazi au intern ijapokuwa kama ni intern nataman iwe hapa hapa Dar es salaam kwa lengo lakuepusha gharama.

Niwe mkwel sichagui kazi ilimradi tu iwe ya halali ijapokuwa itakuwa nzuri sana nikipata katika eneo nililosomea ili niendeleze career yang ila sichagui kwa yoyote mwenye uwezo wa kunisaidia.

Natanguliza shukran na samahanin pia kwa usumbufu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom