Natafuta Kazi Za Hoteli Za Kitalii Arusha

Natafuta Kazi Za Hoteli Za Kitalii Arusha

bbenedict

Member
Joined
Jun 30, 2013
Posts
91
Reaction score
7
Heshima Zenu Wakuu,nisaidieni Jamani Mwenzen Natafuta Kazi Kama Receptionist,housekeeping Ama Nafasi Nyingine Yeyote Za Hoteli,english,french Na Italian Inapanda Vizuri Sana.Contacts 0655042717,ahsanteni
 
Mkuu kwanza Hongera una advantages nyingi kwa kuwa ni Multi-Lingual Staff
Tatizo ni kwamba kwenye amalezo yako hujaonyehsa uzoefu wako na Elim yako juu haya Masuala.
Maana haya hayana kubahatisha kama mamalishe,unasikia lete harage na mchicha mbili.

Hii ni taalum.
Weka wazi upewe njia,na kama upo tayarikufanyakazi Zanzibar basi kuna sehem nitakupa contacts zao uwatumie,lakini uwe na uzoefu tusitiane aibu
 
Ahsante Mkuu Kwa Majibu Yako Ya Hekima Na Busara,mimi Elimu Yangu Ni Form Six With Diploma In Travel And Tour Operations With A Certificate In Airline And Ticketing,ozoefu Wa Kazi- Nimefanya Na Serena Hotels Na Hotel Nyingi Ndogondogo Hapa Arusha Pia Na Tour Companies In Reservations And Bookings/administration.Kiujumla Sijasomea Mambo Ya Hoteli Ila Uzoefu Kwenye Secta Wa Si Chini Ya Miaka 7 Ninao.
 
Mkuu Mimi Sichagui Pa Kufanyia Kazi Ilimradi Tu Huko Zanzibar Wawe Na Staff Quarters Maana Mwenzenu Huko Sina Ndugu.
 
Ahsante Mkuu Kwa Majibu Yako Ya Hekima Na Busara,mimi Elimu Yangu Ni Form Six With Diploma In Travel And Tour Operations With A Certificate In Airline And Ticketing,ozoefu Wa Kazi- Nimefanya Na Serena Hotels Na Hotel Nyingi Ndogondogo Hapa Arusha Pia Na Tour Companies In Reservations And Bookings/administration.Kiujumla Sijasomea Mambo Ya Hoteli Ila Uzoefu Kwenye Secta Wa Si Chini Ya Miaka 7 Ninao.
Nakubali mkuu,unajua Diploma uliosoma inamahusiano ya karibu sana na baadhi ya sehem za Hotel kama
a)Reservations Department
b)Sales Department,hasa upande Holidays Desk(Excursions Desk)
c)Telephone Operator
d)Front Office Depertment(humu kuna viidara kibaoo vimegawanyika,tena vingi sana)

Na kwa vile umeishafanya kazi kwenye Up Market Classes Hotels kama Serena,basi naamini upo vizuri,maana Product za Serena lazima uwe vichwa cha ukweli.

Ngoja nikupe wazo moja ndugu yangu.
Kwa Level yako na uzoefu wako,hembu nenda Pale Mweka Collage kasomee mambo ya Wildlife.Nakuhakikishia ukitoka pale utakula ajira sehem za maana na maslahi mazuri sana.
Unajua Mweka ni chuo kikubwa sana kwa upande wa Africa kwa mambo ya Wildlife,na Guides wote wazoefu lazima upitie pale ili upewe Leseni ya kuwa Kama Professional Guide.

Kuna kazi watu wanaziona za kawaida lakini zinamarupurupu mengi sana.
Hawa Guides wanaoneda na wageni Safaris wakirudi wanampunga mrefu mbali na mshahara.

Mfano hata kwenye Hotels,mie ukiniambia nafasi gani uchukue nakushauri uchukue Housekeeping,maana tips huko kibaoo,na mazagazaga mengine tele wanakuachia wageni,watu wengie wanaona zile kazi za kuukabia pale mapokezi ndio za maana sana na kuona kama House keepers ni wenye elim ndogo,hiki ndio kinawaponza.Wakati wenzao kwa siku wanatengeneza pesa,akikosa leo basi kesho hata dola mbili hakosi,wewe mwenzangu wa mapokezi na sehem nyingine unategemea mshahara tu.
Kwa muono wangu,only tow posts kwenye Hotel zinalipa sana,Housekeeping,Waiting Services.

Hembu tuma CV yako nikuangalizie sehem,ila sio guarantee unajua kipindi hiki sio cha ajira,maana tumetoka July and August ambapo ni the most peak season,sasa ajira nyingi zilitoka kuanzia March.Ila kama kuna sehem ime open up ndio unakuta watu wanapenya hapo.

Wakati huo huo,ningependa kujua kwanini uliacha kazi hizo za awali,na kwanini hasa uliacha Serena Inn.
Usione aibu kusema kama uliiba,maana kuficha hakusaidii kitu,muhim ni kutubu na kusonga mbele,yote ni mapito tu.
 
Ndugu Zanzibar Spices Kusoma Sikatai,shida Hizo Tuition Fees Za Mweka,mimi Ni Single Mother Of Two Na Kujikita Kwenye Elimu Wakati Watoto Wanahitaji Kushiba Ni Ngumu Kwa Sasa Secondly Sijawahi Iba Kwa Kampuni Yeyote Ile Na Kwa Serena Kusema Ukweli Nilidanganywa Na Kidume Enz Za Usichana,nilikua Manyara Serena Kidume Kikanipiga Kiswahili Nirudi Mjini Tuishi.Arusha Kazi Zipo Ila Nimeapply Had Nimechoka Siitwi Kwenye Interview,andbeyond Mnemba Zanzibar Nimefanya Dukani 6 Months Hali Ya Hewa Ikanikataa(kisiwa Cha Mnemba Kina Humidity Sana) Ikabidi Niache.Housekeeping Naipenda Sana,nisaidie Mkuu Nimepinda Mbaya.
 
Samahan ulikuwa unalipwa mshahara kati ya sh ngap na ungependa ulipwe sh ngap?
 
#TUTEER-kuhusu Mshahara Kama Kazi Ipo Hatutashindwana Kwenye Maongezi,mishahara Ya Hotel Za Nafasi Za Kawaida Mbali Na Za Management Si Mikubwa Kivile Mara Nyingi Tunategemea Tip Kwahiyo Tukishika Kichwa Cha Kizungu Tunahakikisha Anapata "a Time To Remember" Ili Atutoe Vizuri.
 
Back
Top Bottom