Natafuta kazi yoyote ya kupata angalau 15,000/= Tsh per day

Aiseeee umenikumbusha mbali sana. Mwaka 2017 nilikuwa nimepigika kinoma. Tukashauriana na mshikaji wangu twende tukatafute vibarua viwandani. Katika pitapita tukatokea kiwanda cha ngano cha mzizima (bakhressa) pale maeneo ya ngozi. Mzee mmoja mlinzi akatuuliza, "vijana mnafikiri kwanini hapa kila siku kazi zipo?" Akatuambia kuwa kazi za mle ndani ni ngumu balaa na kama ni mgeni ikifika saa 5 kuna uwezekano Mkubwa ukaiba nguo zako mwenyewe na kusepa.

Aisee! noma sana mkuu. Ila mimi niko tayari kukomaa kwakua mwili na nguvu ninazo na pia nna uhitaji nayo sana hivyo hakuna namna as long as malipo yasiwe chini ya 15k per day. Wanalipaje pale?
 
Ogopa kazi kwenye hicho kiwanda MALIPO sio km alivyokwambia utaacha siku hio hio uwiano wa kazi na MALIPO haviendani nimekwambia jichanganye k/Koo km una smartphone kajichanganye pale ongea na wale mawinga wakupe ramani utaanza kuingiza Pesa tatizo vijana mnapenda kushikwa mikono kila sehemu kwanini haujiongezi nakuhurumia huko kiwandani unapoenda SIO
✍️

Sawa mkuu, nimekuelewa. Nimemtafuta Flames ila naona bado hajajibu kitu, ngoja niingie site mwenyewe.

Shukrani mkuu.
 
Ogopa kazi kwenye hicho kiwanda MALIPO sio km alivyokwambia utaacha siku hio hio uwiano wa kazi na MALIPO haviendani nimekwambia jichanganye k/Koo km una smartphone kajichanganye pale ongea na wale mawinga wakupe ramani utaanza kuingiza Pesa tatizo vijana mnapenda kushikwa mikono kila sehemu kwanini haujiongezi nakuhurumia huko kiwandani unapoenda SIO
✍️
Kwani hapo kwenye kua winga hashikwi mkono??

Sometimes toeni ushauri tu bila masimango, kubali kua binadamu tumetofautiana, si ajabu unamtia dongo chalii ilhali na ww ulibebwa kwa mbeleko ya chuma.
Sio poa mkuu, wanaume ni kushikana mikono.
 
Aisee! noma sana mkuu. Ila mimi niko tayari kukomaa kwakua mwili na nguvu ninazo na pia nna uhitaji nayo sana hivyo hakuna namna as long as malipo yasiwe chini ya 15k per day. Wanalipaje pale?
Aisee kijana kiwanda gani kikulipe 15k per day?? Labda kama unafanya day & night.

Ujue 15k per day ni salary ya mtu mwenye diploma yake safi kabisa.

Usitegemee makubwa sana, kama huna mishe kabisa tafuta mahali pa kujishkiza ukiangalia ramani zikoje. Hiyo kutaka malipo makubwa kwa kazi usizo na ujuzi nazo utazipiga chini nyingi mkuu.
 
Heshima yenu wakuu.

Ninaorodhesha credentials zangu hapo chini kwa lengo la kuomba kazi ya muda mfupi ama mrefu yenye malipo yasiyopungua 15,000/= kwa siku.

1. Ninaishi Dar

2.Umri wangu ni miaka 23

3. Nina bachelor's degree ya management of social development

4. Sichagui kazi

5. Mzoefu wa kuendesha gari japo sina driving license

6. Nimepita JKT

7. Nna experience ya procurement and sourcing

8. Ware house maintenance

9. Gym trainer

10. Door to door deliveries
Jeshi la polisi linetangaza kazi nenda kaombe vigezo vyote unavyo kuanzia umri Hadi cheti cha jkt kazi ni kwako

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Nashangaa watu wanaodharau mtoa mada kutaka kazi ya 15k kwa siku.

Bandari ya dar es salaam na ukubwa wake wote na kuingiza faida kubwa vibarua wake wasio wazalishani wanalipwa 9000 kwa siku na wazalishaji wanalipwa 11500.

Kwahyo nashangaa mtu anayedharau malipo ya 15k.
 
Heshima yenu wakuu.

Ninaorodhesha credentials zangu hapo chini kwa lengo la kuomba kazi ya muda mfupi ama mrefu yenye malipo yasiyopungua 15,000/= kwa siku.

1. Ninaishi Dar

2.Umri wangu ni miaka 23

3. Nina bachelor's degree ya management of social development

4. Sichagui kazi

5. Mzoefu wa kuendesha gari japo sina driving license

6. Nimepita JKT

7. Nna experience ya procurement and sourcing

8. Ware house maintenance

9. Gym trainer

10. Door to door deliveries
Ukiona sehemu kuna ujenzi nenda kaombe saidia fundi
15000 unaipata kwa siku vizuri kabisa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom