Natafuta kazi yoyote ya halali

Natafuta kazi yoyote ya halali

mwakalindile

Member
Joined
Mar 12, 2017
Posts
16
Reaction score
13
Habari gani watu wa nguvu imani yangu kuwa wote wazima acha niende kwenye maada, jamani mwenzenu huku natafuta kazi yeyote ili mradi tu kuna malipo.

Hadi nimeamua kuja jf, ujue hali ni mbaya suala la kuajiriwa serikalini nilishaliondoa kichwani mwangu yaani laiti nikipata hata kazi yeyote ile at least nikusanye ka mtaji daa ila haya maisha, nimeomba sehemu mbalimbali lakini bado sijapata.
niko mkoa wa mbeya, ni kijana wa kiume

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila la kheri mkuu.

Uwe na subira utapata tu.
 
Una elimu gani mkuu?
Kama una utaalamu na umeme/mechanics japo kidogo jaribu kuchungulia camusat/htt hapo mbeya huwa wanaajiri mara kwa mara japo wanapenda pesa sana maana ili upate ajira lazima utoe 800,000 to 1.0M ila jaribu kila mtu na bahati yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom