Natafuta Kazi Ya Uhausiboi

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
2,030
3,908
Wadau Amani kwenu;
Natafuta kazi ya uhausiboi Nina uwezo wa kufanya yafuatayo:
  • Ninauwezo wa kufundisha watoto wanapotoka shule masomo mbalimbali ya shule kwa lugha ya kiingereza kuanzia primary mpaka sekondari kwani mimi ni mwalimu by profession.
  • Nina uwezo wa kufundisha watoto kompyuta na nitakuja na laptop yangu na kuwafundisha hapo nyumbani kwa sababu mimi pia ni mtaalamu wa IT
  • Nina uwezo wa kuendesha gari kama una gari nitawapeleka watoto shule na kuwachukua na vile vile kumpeleka mkeo sokoni akanunue mahitaji
  • Nina uwezo wa kupika vyakula mbalimbali vya kawaida
  • Nina uwezo wa kufua,kupasi
  • Nina uwezo kufanya gardening na landscaping
Kwa hakika ukinipa ajira utapata faida ya kipekee sana.

Mahitaji yangu ni kama ifuatavyo:

  • Kwanza uwe na servants house inayojitegemea,makazi yako yawe maeneo ya masaki,mbezi beach au maeneo kama hayo ya high end
  • Mshahara ninaotaka ni wa shilinging 120,000 tu
  • Kula itakuwa ni juu yako
  • Utanipatia bima ya afya ya NHIF
  • Mshahara wangu utanilipa kupitia bank akaunti kila mwezi
Kama kuna mtu aliyeko maeneo hayo na anahitaji HAUSIBOI aliyekamilika basi anitafute PM

Nimechoka kukaa kijiweni mwaka wa tatu huu sioni dalili za ajira za kipedeshee naona nijaribu huko

Nitahitaji mkataba wa miezi sita sita.

Asante
 
Mi nimekuelewa kabsa, mazingra uliyochagua sitatia neno, mana kila mtu ana priorities zake. Kwa mshahara unaotaka na ujuz/uhitaji/utayar wa kufanya kazi hizo upo sahihi kbsa, tusipinge ukweli kama wahudumu wa nyumbani nao wana level zao kutokana na huduma anazoweza kuhudumu, basi lazma mishahara itofautiane, mfano lundo kubwa la wahudumu weng wa kazi za ndan wa ktz au kiafrika ni bora mfanyakazi, yani awe tu anaweza kupika, kuosha vyombo, kumbembereza mtoto anapolia na vikazkaz vingne vng vya ndani sijui kudeki, kufua n.k. Hao ndo weng wao mishahara ni elf 80 kushuka japo napo still sio fair ila ndo ukweli huo, mfanyakaz wa ndan kama huyo huwez mlinganisha na mfanyakaz wa ndani ambaye sio tu anaweza kumbembereza mtoto anapolia, bali anaweza kutoa full care kwa mtoto mdg mfano kumfundisha kama kumwelekeza home work, kuhakikisha halii(kwa sababu inayoweza kuzuirika) sio wale kila saa utashkia " nyamaza" kumpa furaha, kupika chakula bora na vya aina mbali mbali na si bora chakula sio wale wa dagaa, ugali, maharage na wali, kupeleka watoto shule kwa usafr kama hvyo wewe, si yule akiwavusha barabara tu utaskia haya kimbieni, na mambo mengne meng ya kitaalamu. Sasa mtu kama huyu huwez ukampa nae elf 80. Kwa ufupi upo sahihi ila tegemea mapovu ya sisi waganga njaa, wenye kejeli na frastruation zetu.
 
mimi ni mwalimu by profession.
Dah pole sana mdau!

Kuna kipindi najiuliza sisi kama taifa tunaeleka wapi? Nikutakie kila laheri mkuu ila ningependa kukupa mawazo kama fuatavyo...

1. Sasa hivi vijana wamemaliza masomo, kwanini usitafute twishwn center ukafundishe?

2. Umesema una laptop kwanini usiuze alafu ukapiga mishe za biashara au kilimo!!

Anyway, Mungu akutangulie kiongozi...
 
Vyuma vimekaza aisee... mwalimu professional anataka kuwa house boy... Tunaochukua hii bachelor of education mnatutisha aisee
 
Tuma picha yako kwanza ili nione kama unaweza kuwa threat kwa binti yangu na mke wangu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom