Mkuu Elia hongera kwa kuweza kuchukulia fani ya urembo serious, natumaini utakua umeiva kweli yaani mtaalam kweli wa kudesign nywele.
Ushauri wangu kama kunakazi tayari umefanya ambatanisha picha za watu uliwatengeneza nywele.
Kumbuka kuficha taswira ya mtu wengine hawapendi kutumika katika matangazo
Hii itakusaidia kwani mtu tayari atakua ameona ufanisi wa kazi yako
Pili ikiwa unaendelea kusubiri kupata kazi ya mtu akutume.Wewe anza kwa kutengeneza wigs mbali mbali kama za rasta, croshet, na mawigi mengineyo halafu
tafuta wateja wako mtandaoni kwa kutumia simu yako.
Wateja wako wanapatikana maofisini mpaka wa mama wanyumbani .
Mtaji wako unaanzia elfu 10, kutengeneza pesa zaidi ni jinsi ya wewe utakavyoweza kusimamia na kuboresha ujuzi wako.