Natafuta kazi: Part time teaching/tutoring job

Natafuta kazi: Part time teaching/tutoring job

Diwani

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2014
Posts
2,825
Reaction score
3,021
Habari Waungwana.

Naitwa Diwani D.A. nina umri wa miaka 27, kitaaluma ni Mwalimu, nina uzoefu wa kufundisha tangu mwaka 2019. Nina uhitaji wa kazi ya kufundisha kwa muda (Kutwa), Shughuli hii inaweza kuwa Shuleni, nyumbani, Ofisini ama kwenye taasisi yoyote ambapo Mwanafunzi "Learner" atapata muda wa kujifunza kwa takribani dakika 60 kwa kipindi.

SIFA (TAALUMA & UJUZI)

- Elimu yangu ni Shahada ya Kwanza ya Elimu katika Saikolojia. (B.Ed Psychology)-2019

- Elimu ya Matumizi ya Awali ya Kompyuta ngazi ya Cheti; kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) - 2014

UJUZI - (Nafundisha pia)

-English course and Programming; Kwenye Mashule na taasisi, ama Watu binafsi wanaotaka kujenga ari ya kujifunza Kingereza kwa "Level" zote yaani; Basic, Intermediate and Advanced.

- Matangazo ya Mitandaoni (Social Media Marketing) - Self taught and experienced.

- Kutengeneza Maudhui ya mtandaoni (Content creating for Social Media - Branding niche) nina uzoefu na Nafundisha pia. Nimefanya kazi na GEW Tanzania.

- Communication Skills for Customers care officers. (Elimu ya Mawasiliano kwa maafisa huduma kwa Wateja)

- Freight (Clearing)

- Ni Mwalimu wa History, Literature in English.

Napendekeza Part time kwa sababu ya shughuli nyingine nifanyazo; ingawa hazitanifunga endapo nitapata Full time.

Mawasiliano: 0743123946

Natanguliza Shukrani.
 
6E83D1B1-2CC2-4479-B3D4-6973BB01100F.jpeg
 
yaani ukisikia mwanzo mgumu ndo huu,, kila la kheri walimu wa nchi yetu.
 
Hivi posho ya laki kwa mwezi kwa maisha ya sasa ipo realistic kweli?
Ukiona hivyo wamelenga hasa wanao ishi maeneo yaliyopo ktk wilaya husika

Au kama una ndugu basi upate kwa kuanzia

Wasomi siku hizi wame eneo kila wilaya, kata na vijiji... hasa kwa fani ya walimu

Na hao wana lipa kwa mapato yao ya ndani
 
Ukiona hivyo wamelenga hasa wanao ishi maeneo yaliyopo ktk wilaya husika

Au kama una ndugu basi upate kwa kuanzia

Wasomi siku hizi wame eneo kila wilaya, kata na vijiji... hasa kwa fani ya walimu

Na hao wana lipa kwa mapato yao ya ndani
Sure
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom