Hata mimi nimeshtuka na kushangaa sana. Fikiria msomi wa shahada anashindwa hata kujitambulisha na kujieleza juu ya nafasi ya ajira.
Ameshindwa kabisa kujiamini juu ya ujuzi wake na anaona kama hauwezi kumpatia ajira hapa JF.
Ameshindwa kabisa kujieleza kuwa hiyo shahada yake inaweza kumuwezesha kufanya kazi gani na gani na kwa ofisi zipi ziwe binafsi, mashirika au hata miradi ya kiserikali.
Ameshindwa kabisa kuwaeleza watu wanaofanya biashara ya Real Estate umuhimu wa kampuni zao na ofisi zao kuwa na mtaalamu kama yeye.
Ameshindwa kabisa kujieleza vyema kama msomi badala yake anatafuta huruma za watu hapa na kazi za ukiwa na akili timamu. Hili linasikitisha sana, sasa kwanini alienda hiyo shule?
Mleta uzi rudia kuandika kitu kinachoeleweka.