Natafuta kazi inayohusiana na Taaluma yangu (Mipango miji) au kazi yoyote itakayofanya niishi na kuendesha maisha yangu

May 20, 2020
34
66
Wanajukwaaa la ajira na tenda heshima na iwe kwenu.

Mimi ni graduate katika fani ya Mipango miji na vijiji ya chuo kikuu Ardhi (ARU)

Nipo mbele yenu kuomba yeyote yule mwenye connection na kazi yoyote inayohusiana na Taaluma yangu (Mipango miji) au kazi yoyote ambayo haikinzani na sheria za nchi aweze kuniunganisha au kunipatia.

Aidha, baada ya kuhitimu masomo yangu nimekuwa nikifanya kazi na Taasisi binafsi. Pia nimeweza kujitolea katika halmashauri mbalimbali ili kupata uzoefu zaidi.

Hivyo, Kwa yeyote mwenye uhitaji anaweza nicheki PM Kwa mawasiliano zaidi.

Ahsanteni.
 
Ila ulijaribu kuomba zile za utumishi serikalini za MDA&LGA kuna nafasi kama 800 hivi za kada yenu mkuu jaribu na huko mkuu.
 
Mkuu si unaweza kuaanda Mipango ya Miji Mipya kisha Ukauza.Kama vile wale waliondaa Mpango wa Kigamboni ingawa uliingiliwa na shubiri?

Ni wazo tu ila nakutakia kila la heri katika utafutaji wako.
 
Ahsante!
Kule nimeomba na ni nafasi Tisa (9) za Town planner bila shaka nafasi 800 ni za maendeleo ya jamii

Ahsante Kwa ushauri mkuu mzuri, japo changamoto huja kwenye kutwaa eneo kwaajili ya kupanga na kupima. Utatakiwa uwe na Fedha ya kununua eneo au uingie mkataba na wamiliki wa asili.
 
Mkuu,Kuna Planning stages nyingi.Kwanza unaaza kwa kuandaa Paper work/proposal ya eneo unalotaka kulifanyia planning na jinsi ambavyo unataka liwe mfano,Roads,Public Spaces/Waste Disposal,Commercial,Social etc.Baada ya Hapo unaonesha Total Space itakuwa na Ukubwa gani.

Residential Planning unaifanya iwe full yaani inaonesha aina ya nyumba idadi ya occupancy na gharama za ujenzi wake.Vile vile unafanya hivyo kwa kila eneo ambalo unataka liwe sehemu planning yako kisha ukishaandaa andiko lako unalivunja katika vipengele husika kisha unalipeleka kwa wadau kama vile financiers,policy makers,investors etc kwa lengo la kutawaomba waingi makubaliano na wewe.

Baada ya hapo ukiwa na full paper work unaazana kugonga milango kwa wadau kama vile matajiri,wamiliki wa maeneo,wafanyabiashara,mabenki etc ukiwaalika kuwekezakatika huo mji wako.Unaweza kuupa Jina kabisa ila bila kuwa na location.Tena ili inoge zaidi unatafuta kabisa na kampuni za ujenzi kwa ajili ya kukupa mwongozo wa bei za ujenzi wa barabara,nyumba na majengo mengine.Kisha unaendelea kugonga Milango

Sasa wakati unagonga milango utakutana na wanaoweza kukuajiri kwa sababu ya kuona drive na uwezo wako na pia unaweza ukapata fursa ya kupat mtaji.

Bado tu sijakupa mwanga?
 
HOngera sana Town Planner, turudi shule. Nimeona tangazo UN wanakuja kujenga ofisi zao Bongo
 
Nashukuru Sana mkuu.

Hakika baada ya kusoma hii comment kuna nguvu fulani hivi ya upambanaji nimeipata na kujiona nimebweteka katika kuitendea haki taaluma yangu.

Ahsante na ubarikiwe.
 
Back
Top Bottom