Natafuta kampuni ya uchimbaji kisima

Natafuta kampuni ya uchimbaji kisima

Akurutogo

Senior Member
Joined
Aug 29, 2013
Posts
199
Reaction score
103
Natafuta kampuni ambayo ina uwezo kuchimba kisima maeneo ya Moshi bar karibu na relini njia ya kuelekea Kampala university. Nimechimbiwa na waswahili wenzangu visima 2 lakini yamebaki mashimo tu kwa sababu kwamba wanapopata maji wakiingiza Compressor inapasua bomba hivyo kusababisha graves kuingia ndani na kusababisha kiwe kifupi. Mfano nilichimba cha mitandao 80 mara ya kwanza nikapata maji nikitumbukiza pump inavuta kw muda mfupi kama lita 100 then yanaisha, nimechimba cha 2 mita 90 kikawa na maji lakini walipoleta Compressor inapasua plates za ndani na kusababisha kokoto kuingia ndani ya kisima na kukifanya kifupi cha mita 60 tu. Naomba kampuni ambayo itanisaidia kufufua kimojawapo ya hivi vilivyopo au kuchimba kingine kipya. NAHITAJI WATU WENYE UTALAAMU NA EXPERIENCE si wenye experience peke yake kwani wamshanitia hasara na maji nahitaji sana
 
Back
Top Bottom