Natafuta Gari aina yoyote ndogo

Dah aisee wewe mkuu ni noma, sijacheka tangu asubuhi.
Lakini hakuna lisilowezekana chini ya jua.
Ushauri wangu tu endapo utalipata kuwa makini nalo sana unaweza ukajikuta cheti cha kuhitimu mafunzo unapewa ukiwa tayari umeshafika mbinguni
 
Wasikukatishe tamaa mtu wangu,
Jichange change ongeza siku zako za malengo angalau ifikie 350 upate hata starlet grenza
 
Mleta mada ongeza angalau ifike 2-2.5, mwaka juzi Gx 100 tumeiuza kwa 2.5 m. Ilikua nzima, mimi binafsi nimeitumia. Lenga watu wenye parking iliyo shiba yani anakuuzia huku ukiwa unamsaidia kusafisha parking yard yake. Ila ukiongea na tia maji tia maji ata mkweche atakukomalia kwa bei kubwa ili akatatue shida zake bahati mbaya humu ndiyo wapo wengi na wanaleta kejeli.
 
Dah aisee wewe mkuu ni noma, sijacheka tangu asubuhi.
Lakini hakuna lisilowezekana chini ya jua.
Ushauri wangu tu endapo utalipata kuwa makini nalo sana unaweza ukajikuta cheti cha kuhitimu mafunzo unapewa ukiwa tayari umeshafika mbinguni
Kwahiyo nifanyeje wakuu.
 
Mkuu kunakitu nimepata zaidi. Nitaanza kuzunguka yard nyingi ila hiyo yenu huwezi niuzia kwa bei ya kupoa kidogo.
 
Shida nikiwa na kitu kipya hata kukitumia mwenyewe nakua na wivu ndio maana nahitaji kwanza nizoee gari ambayo hata nikipogwa pasi namwambia fresh tu haina noma ndio mambo ya barabani
 
Your Genius bro
 
Shida nikiwa na kitu kipya hata kukitumia mwenyewe nakua na wivu ndio maana nahitaji kwanza nizoee gari ambayo hata nikipogwa pasi namwambia fresh tu haina noma ndio mambo ya barabani
Kiongozi hata uwe na magari kumi,
Hata uwe na uzoefu wa miaka kumi.
Gari jipya ni jipya tu hata likiwa mkweche.
Matatizo mengi ya barabarani kwenye nchi yetu hii ya Tanzania yanasababishwa na haraka.
Kama unahofia kupigwa pasi pangilia route zako vizuri utoke mida ambayo hamna foleni mpaka utakapolizoea gari lako.
Kuna mdau kashauri ujichange mpaka 2.5, hapo mimi ningeshauri katika hiyo 1.5 utoe kama laki nne. Uende kujifunza udereva kwenye chuo sahihi, lazima kulikua na bajeti ya mafuta.
Tumia bajeti hiyo ndani ya mwaka utakua unakaribia 2 fulani hivi.
kumbuka usalama ni muhimu kwako na kwa wenzio. Usijifunzie gari barabarani bila taratibu sahihi.
Kwa kumalizia kuna sehemu nilisoma, takwimu zinaonesha wamiliki wengi wa magari kwa mara ya kwanza, mara yao yanahusika kwenye ajali (kubwa au ndogo) ndani ya miezi mitatu ya kwanza.
Nyingi sio wao waliosababisha, kwa hiyo hata ukiwa makini na mwenye uzoefu haimaabishi utakaye mruhusu atoke na gari lako atalirudisha salama
 
Mkuu kunakitu nimepata zaidi. Nitaanza kuzunguka yard nyingi ila hiyo yenu huwezi niuzia kwa bei ya kupoa kidogo.
Imeshauzwa mkuu.. nilipo sema yard sikumaanisha hizi za kibiashara. Mfano ukiona jirani ana magari mengi. Angalia lile kuu kuu muombe aku uzie. Kama huna jirani wa hivyo jaribu kuulizia kwa watu wako wa karibu. Au jaribu kuongea na mafundi garage waku link na maboss wao. Gari kwa 2m-2.5m unapata vizuri sana, ukibahatika unaweza pata zuri ingawa most likely linaweza kuku cost kwenye maintenance. Kila la kheri mkuu
 
Asante mkuu. Kwahiyo ninunue tu ya malengo safari iendelee
 
Asante mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…