Codename96
Member
- Sep 17, 2020
- 90
- 85
Asante sana ndugu kwa ushauri.Subiri Serikali ikirelease majina, kuna magepu yatapatikana. Pia katika sector ya Elimu mwezi wa kumi na mbili ndio huwa na kazi nyingi.
Kwa kweli sikati tamaa kaka.Usikate tamaa
Siwezi kuwa na amani ya usingizi. Stress tu yani!Ujalala tu.
Ndio
Ofisi yao iyo Gardaword ndio pale Mikocheni Warioba ukitokea Scott Pizza.Mkuu omba kazi ya ulinzi
Kwa mwezi 250k unachukua bila wasi wasi
Nenda mikochen wanachukua hadi sasa
Unafanya kazi saa 12 tu unatulia
Kana upo tayar, fuatilia ndan ya Wiki tatu utakuwa umeshapata kazi, bila hata kuwa na connection wala nini
Ni juhudi zako tu
Acha upotoshaji wewe.#Correction: Matokeo ya semester 5 hayana transcript. Hiyo uliyonayo ni provisional results.
Alafu rudi nyumbani kwanza. Hakuna uhusiano wa maisha ya kitaa na degree yako, ukitaka kujitegemea kajipange tena upya hapo ulikuja kwa ajili ya kusoma sio kutafuta maisha.
Tatizo mkijaga mjini mnaishi maisha ya season kias kwamba hata kurudi nyumbani mnaona jau maana mlishanyea kambi.
Nasisitiza rudi kwenu kwanza.
Ajira katika shule binafsi kwa kiwango kikubwa zinapatikana Dar es salaam, usijaribu kutakaka kurudi kijijini kama kweli unahitaji ajiraHabari za muda huu.
Ndugu zangu mimi natafuta ajira ya ualimu maana maisha hapa Dar es salaam ni magumu sana.
Mimi nilikuja Dar kwa ajili ya chuo tu kwahiyo sina hata ndugu sasa chuo nimemaliza na sina shughuli yoyote.(sikusoma kwa mkopo).
Kijijini kilimo ni cha jembe na hata nauli ya kuendea tu sina. Naishi kwa madeni.
Natarajia kuhitimu degree ya ualimu mwaka huu.
Nina transcript ya matokeo ya semester 5.
Nikipata ajira ya angalau kuniwezesha kulipa kodi na madeni ya gharama za maisha ntashkuru sana.
Ingawa nimetaja Dar es salaam, niko tayari kwenda mkoani ikibidi.
1. Kiwango cha elimu: Natarajia kumaliza BAED mwaka huu hivyo sina cheti, nina transcript ya matokeo ya semester 5.
2. Masomo ya kufundishia: Historia na Kiingereza.
Asanteni. Kama kuna swali lingine ntafurahia kulijibu. Niko tayari kwenda mkoani ikinibidi.