Habarini wanajamvi,
Nahitaji fundi wa kushona nguo kwa kutumia cherehani (fundi
cherehani/tailor), awe amehitimu mafunzo yake vizuri japo sitaangalia
vyeti bali uwezo wake katika kushona nguo yenye kiwango kizuri, pia awe
mbunifu isiwe kila kitu aangalizie desa mahali. Nitamuhitaji fundi huyu
kwa kazi maalumu kwamba anapofanya kazi yangu asiwe na viporo vya mtu
mwingine, na atalipwa siku hiyo hiyo kuendana na kazi aliyokamilisha.
Kwa fundi mpya aliyehitimu akiwa hana vifaa atapewa vifaa vyote ambavyo
ni bure wala hatakatwa ktk malipo yake.
Kama una ndugu au rafiki unamfahamu tafadhali nitumie pm ili tupeane
mawasiliano.
NB: Nahitaji fundi aliyepo dar es salaam.