Nimekuwa nikitafakari juu ya mgombea wa CCM kuitwa/kujiita tingatinga kwa maana ya mchapakazi. Ni kweli tingatinga ni mashine inayochapa kazi sana, inang'oa miti inasawazisha makorongo na hata kuporomosha vilima. Tingatinga linaweza kujaza udongo, mchanga au mawe kwenye lori kubwa ndani ya dakika chache. Tingatinga ni chapakazi!! Lakini tingatinga linaweza pia kubomoa nyumba, barabara au hata madaraja likielekezwa huko. Tingatinga ni haribifu pia. Kufanya yote tingatinga linamtegemea dereva wake ni nani. Dereva wa tingatinga aweza kulitumia vizuri au vibaya. Ninachojiuliza ni huyu bwana anayeitwa tingatinga dereva wake ni nani? maana huyo ndiye atakayelifanya tingatinga lisaidie ujenzi au ubomoaji. Tutafakari pamoja, nani dereva wa hili tingatinga? je tulinunue au tuliache?