Nastaafu kuuza wake za watu Pt2 (Ijue hii biashara nje ndani)

lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,700
29,160
Igweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee! Poleni kwa kuchoma mahindi, la kumshukuru Mola leo tumeendelea sio kuendekeza lawama za kwanini nilipotea.

The Gay Client.
Sasa nikiwa na muwaza huyu mtu mzima anaetaka kuuzwa kwa hiari yake, sijampatia mteja nakuna kichwaaaa, nikakata shauri nikamsimulie kaka mmoja hivi mchizi wangu. Huyu kaka mimi nilikuwa nimemzoea coz kwanza si mchoyo kabisaaa, afu mcheshi na anapenda kutukana kama mimi tu. Tukajikuta tumezooeana.

Nikampigia akitoka kazini tuonane, namjua anajuana na watu ni balaaa. Asingenikosea tajiri wa kututoa na mtu mzima wangu kule. Kufika baada ya salamu nikampa A to Z, bwana mimi sahivi nauza watu mjini hapa, maisha magumu, sasa nataka unisaidie kwenye swala la marketing ya hii business.

Kwanza akagunaaa! Akaniambia yaani bora nilivomwambia nikasema mteja keshapatikanaaa. Akaniambia nikwambie siri, ukisema nakuua. Tobaaaa! Nikajua yeye ndo anamtaka huyo mtu mzimaa. Nikasema kwani kitu gani, nitamuuzia tu, maadamu bei ifikiwe.

Akaniandikia kwenye simu, kutamka aona hayaa. "Nitafutie bwanaaa" Tobaaaaaa! Nikajua alitaka kuandika bibi mkono umeteleza. Akanikazia jicho, "Im gay!" Tobaaaa! Ndo nilivozaliwaaa! Mxiuuuu! Kunikata maini akaniambia usijifanye mwema, dakika kumi nyingi ulikuwa unauza mke wa mtu, mbinguni huendi leo wala kesho. Mmmmmmh! Lakini kweli. Nikajikaza, nikamwambia nishakuhisi wewe, muone kwanzaaa. Tunagonga kabisaaa.

Ukistaajabu hilo alikuwa na girlfriend kabisaa kazaa nae mtoto mmoja. Business ikawa ngumu kabisaaa. Mali mbili zote hazieleweki. Nikamfata msengery mmoja saluni kinondoni, anatusuka. Kufika kule namkuta na bible! Tobaaa! Nikamvagaa kwa mashamu shamu nikajua hakosi mabasha wawili wa 3. Akaniambia Lara nimeokokaaaa! Njoo kwa Yesu. Mmmmmmhhhh! Nimeoa sahivi, nina mtoto. Ikabidi nikae chini nimsikize.

Shoga ganiii aloekuwa ananipata Kinondoni hiii, achia Aunt Kessy na Aunty Assu? Nimetembea na wabunge, mawaziriii, wakurugenzi, warabu mpaka wa Yemen, Wafaransa, wajerumani, wagiriki, waturuki, warusi mpaka watalianoooo. Muhogo gani nisio ujua mimi wa zamani? Atoke shoga dsm hii anaenipata. Mmmmmh!Nikamwambia wewe mamba yaooooo, hakuna aliekupata shosti, kisa cha kuokoka? Na kuoa na kuzaa ndo sielewi.

Ananiambia Lara1, nilibakwa mwenzio, kuna mwanaume alinichukua kumbe wako lundo sikumbuki idadi, wanadai nilimlia mwenzao hela afu nikamkimbia. Wakanibakaa, wakanibakaaa, mpaka nikazimiaaa. Wakaniwekea chupa za kusaga na super glue. Nimeumwa nusu mwaka. Nilivoamka nilijisalimisha kanisani, ndo wakanipeleka hospitali yao Moshi kufanyiwa upasuaji. Hapa nilipo nimeathirikaa. Baada ya kuchungulia kaburi nikamtafuta Mungu, nashukuru nimempata, mke wangu nae ni mgonjwa tulikutana kanisani, ila mtoto sio mgonjwa. Tunatumia dawa na kufata masharti.

Nakuhakikishia furaha na amani niliyonayo sahivi ni mara laki moja maisha ya usengery.japo nilikuwa star naimbwa na maband, naalikwa kichen party ila ndani nilikuwa mtupuuuu. Sitaki kufa kama Aunty Kessy, msiba ulikuwa na mashoga wachache wasio na stahaaa, ukimwi ulimmaliza akiwa mdogo, nasikia na Aunty Asu alibakwa ameokokaa, na kaoa. Achana na duniaaa, mrudie molaaa. Hela za shetani ni adakadebla, leo unazo, kesho hunaaa. Mmmmmmmmmh! Mazitoooo.


The Rich Wife.
Basi baada ya kuachana na Aunty Mo, nikawa nimekosa pozi kabisaaa. Maana kama ni ushetani, yule alikuwa PROFESSIONAL kama sio AGENT kabisaa. Nae kanawaaa, kamrudia Molaaa! Mi nasubiri nini? Dunia inaishaaaa, nikaona inaisha mda si mrefuu. Nikajisalimisha kanisani. Sikutaka kwenda kanisa letu la Roma maana wananijua wana jumuiya, itakuwaje sasa. Uszuri makanisa yako mengi, nikaenda la nje ya kwangu tu la hawa protetistants. Nikawa naenda tu jioni, sijitambulishi wala nini.

Mara pasta kanikomaliaa, nikajitambulisha robo. Ikafika mda wa kuongea na pastor, maana aliniganda nimeoneshwa unataka kutubu unataka kutubu.Nikamsimulia juu juu tu uhusika wangu kwenye dhambi za wengine. Nikapata amani, nikajua yameisha. Mara mama mmoja akataka kunizoea kwa kasi sanaaa. Mmmmh! Nikapata mashaka mjini hapa, mmama mwenye mihela anizoee kimpango gani? Afaidike nini? Ila coz ni kanisani nikaamua nione mwisho.

Pastor nae akawa anatumia nguvu nyingi sanaa kunikutanisha na mama. Oooh mama atakusaidia huyu ni bosi anajuana na wakurugenzi ana network kubwa atakusaidia kupata kazi nzuri. Mmmmmh! Weeee! Mwenyewe born here here nikajua tu there is a catch btn me, the woman, and pastor sema sikujua what was it yet. Nikaplay along.

Siku ya siku mama akanipa live, nimtafutie dogo dogo atamhudumia kila kituuuu, atampangia nyumbaa, atamuewekea kuila kitu na gari juu, ila yeye awe anaenda kulala humo wanafanya yao maana mumewe ni mtu mzito mjini hapaaa. Hawezi kuingia guest kimaandazi. Akanipa live tu kuwa pastor kamwambia hio kazi naiwezaaaa. Mmmmmh! Pesa ipo.

Nikasema sasa haya majaribu. Nikaenda kwa tax dreva mmoja namjua ana njaa kisheni na ndo business zake kuichuna mijimama. Akaniambia yeye kaoa sahivi, mkewe mpare mkorofi kishenziiii, lakini sio kesi, mtu atapatikana, na kazi ataifanyaa. Mradi mgao apewe. Kwanza ana ndugu yake kamaliza chuo hana kazi. Akampigia kaja pale nikampa A to Z, akawa anawaza na kuwazuaaa. Mi nampelemba atakupa gariiiii, sijui umenisikia hapo kwenye njiii, nyumba nzima anakupangia, furniture za kisasa, unalelewa mjini ufanye kazi unayopenda kuifanyaaa bila hata kulipwa. Tax dreva nae anachombezaaa hatarii.

Jamaa anasita tu, kukoleza nikamwambia ni ka sexy mama, sio jimama. Kama Zari hivi. Mmmhhh! Njaa anayo ila balls za kufanya hio kazi ndo akawa anawaya waya. Nikamwambia nakupa wiki fikiria. Wiki haikuisha akanipigia niko tayari. Nikamuuliza taxdriver imekuwaje, akaniambia nimemuwekea masharti magumu huku home, nimemwambia na wife amnyanyase mpaka akili zimkae sawa awe mwanaume akaifanye kazi ya kiume. Basi akaenda ofisini kwa maza, maza akawa kamielewa, ila yeye zile adabu adabu za kijijini na aibu aibu ndo zikawa zina mcost.

Maza katoa hela, nyumba ikatafutwa kinondoniii, nyumba elekeziiii, kodi 400,000 ya peke yake enzi hizo lakini. Tulipiga hela ya udalali hapo. Tukapiga udalali wa gari, akamnunulia Gx 100. Sasa ikabakia upande wa dogo kufanikisha. Siku hio alivohamia maza akasema atakuja asuhi yake, tukishaweka furniture, tukala tena udalali wa furniture. Tukamkalisha dogo mpaka saa 8 usiku tunampa pointers. Asituangusheeee. Akomaeeee, akaze. Tax driver ndo akawa kadataa anajilaumu kuoa ile kazi angeifanya yeye. Anamwambia kumshughulikia jimama kama anaingia kaziniii, asijivungeee, ampee mambo ya hatariii, apige mpaka dekiiiiii, chumvini kokote atako taka jimama dogo apige kazi. Niliongea siku hio mpaka nikajihisi kuzeeka. Tukamwambia sisi ndo tunaondoka, tushamfikisha nchi ya ahadi, ashindwe mwenyewe tu.

Ooooooooh! Kazi kaiwezaaa. Fresh mpaka leo mwaka wa 3 sijui wa 4 yuko na jimama. Mpaka kazi alimtafutia kaanza meneja. Yuko mbali mnoooo. Na kanisani sikwenda tenaaaa. Nikawa back in businesssnand rolling.

Huku na huku mdogo wangu akaniambia wake za watu wana group lao la wake za watu la watoto wa kishuaaa. Ananipa stori wake wa maboss walivo na stress. Nikamwambia ni add. Akakomaa siwezi mpaka uwe mke wa mtu. Nikamwambia acha uboyaaa, watajuaje sio mke wa mtu, embu ni add mie hukooo. Akani add. Yalaaaaaa! Patamu hapo!

Mke Kinganganizi!
Nikawa nawachora tu, habby hiki, habby kile, wanajimiminaaaa. Nikamuuliza mbona sioni victim wa stress humj? Wote wako eden. Akaniambia we tuliaaa, sikilizia. Nikawan nimepozi nangoja May day ilie, niseme nae mhanga inbox. Mayday halii, nikawa namsimulia mtu niko group moja. H, la wake za watu, wanabahati, mambo yao supaaa, mambo byeeee, hutoamini. Wana house girl 2, ama 3 kila mtu, mwingine kazaa mapacha kaajiri nurse, yule wa hospitali. Sasa huyo shoga angu hana jemaa, akaanza kuponda, huyo nesi maybe wale wa nguo za kijani. Hahahahaa! Na hao wake za watu hawawezi jisema mule kwenye group, wanajitutumua tu, sasa ukitaka kuwapata undani wao wafate inbox, jifanye mumeo anakusumbua hatari waombe ushari watafungukaaa. Tena anza na huyo alieajiri nesi ushuzi. Hahahaa.

Nikarudi nikamfata mamy nesi inbox, hi, i admire your life so much in the group, naomba nishauri. Mume wangu maluuniii, hafai. Malaya mbwaaa. But i want to save my marriage
, sitaki kuwa divorced and start my life all over again. blah blah blh! Kwanza nikahisi hatojibu. Siku ikapita, nikajua hatojibu, siku ya pili usiku akajibu. Pole!Neno moja afu basi. Nikaendelea kujimiminaaaa. Hakujibu tena. Kila siku namtumia kistory cha uongo uongo, hanijibu.

Siku hio nikamwambia i am living my husband tomorrow after carefull thoughts and all, thank you for being there for me when i needed you most. Nawatakia nyie maisha mema, mnusurikiena husdaa. Akpigaaa! Usiondokeee, hold on, being married is everything believe me. Watu kibao they wish they were us, lakini ndo hivo tenaaa. Wanaume wote wasumbufu, vumilia tu, hata wangu he is barely home, kama naishi mwenyewe tuuu, ndo maana naamua kubeba mimba mfululizo ili nisiwe bored but i was raised better, i can live my home and kids, for better for worse, blah, blah blah. Nikasema BINGOOOOO!

Nikamwambia thanks for the advice. Nikamtafuta 3 or 4 times afu sikumtafuta tenaa. Ikapita miezi 2. Siku hio kanianza. Naona mambo yamekaa vizuri, you aint desperate anymore. Hunitafuti tenaa. Good for you. Nikamwambia im telling you a secret, i am cheating on my husband with this guy. He is so sweet. you wont believe. Akanipigia. Noooo waaaay! Nikampanga pale, nikamwambia im so happy, i dont notice his flaws anymore. I am too busy being happy! Really! Nikamwambia you wont believe it saved my marriage. Basi ndo kunisimulia mume haonekaniii kabisaa n she is convicied ana nyumba ndogo, yet still she must stay married except she is damn miserable. Nikamwambia he has a friend! Akajifanya no waaaay! Thanks lakini.

Basi akawa kila siku anauliza how is it going with the side dude. Nikasema asintanie. Nikamafata mchizi wangu mmojaana vyeti vizuriii, sma ndo anafanya kwa wahindi. Afu ni model wa part time, ana body flani amazing, nikampanga kuna mke wa mtu yupo too modest kukupa hela, lakini atkupa mchongo wa kazi ya maana na connection za msingi. All you have to do is to pretend you are interested and give her attention. Ile problem ya mademu kukuomba hela na kununua K imefika tamati, this is free K. Nikampa namba.

Siku si nyingi bi dada kanitafuta huku kunipa ubuyu, you wont believe i met somebody. Na mie namchombeza kama sijui, he is model i am considering to have an affair with him, i will be such a slut. Huku na huku katoa mzigo, wakaendelea fresh tu, mpaka kamfanyia mchongo kai nzuri tu ya marketing kampuni hizi za simu. Yani katoka kimaisha. Mpaka leo namashaka wanaendelea na yao. Tobaaaaa

Mume Mnyongeee
Nikiendla na kazi hii, siku nikakutana na mchizi wangu tuliefanya nae kitamboo, kachokaaa, kachakaaa, anauza mkaaa. Mchii huyu alikuwa mtu na baa yake, bosi wangu in short ofisini, kila siku ana safiri. Alikuwa na mke na watoto wa 3. Ndo kunisimulia maisha yamempiga alivosimamishwa kule. Kinachomuuma mkew amebadilika hatariiii, anamnyanyasa na balaaaa, mpaka anauza mkaa sio mchezo.

INAENDELEA KESHO
 
Last edited:
Jamaaaaniiiiiii daah!!!!mijicho imentoka mwenzio daaah!!!!ndo nini kukatisha tenaaa..... lara 1
 
Yaani hili movie la leo lilivoanza kwa advertize? Sijui kama hatujakesha tunasubiria part 3!
Kweli hii mtoto hatumwi dukani.
 
lara inaonekana wewe ni mjanja lakini ukibananisha na mandingo unakuwaga mpole sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom