GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Kwanza nikiri kabisa kuwa nimekuwa ni Mshabiki, Mpenzi na nashukuru Mwenyezi Mungu kila mara moyo wangu umekuwa mgumu sana Mimi kuchukua kadi ya Uanachama ya Klabu ya Simba kwani hapa tu siyo MWANACHAMA naumia hata nataka KUFA kwa Presha je ingekuwaje kama ningekuwa MWANACHAMA halali wa Simba?
Japo sijawa bado Mwanachama ila nikiri kuwa NIMEKUWA nikishiriki katika shughuli mbalimbali za kuifanikishia Simba ushindi huko nyuma na hata kwa miaka hii minne ( 4 ) huu sasa unaenda wa tano ( 5 ) nimeteseka sana juu ya Simba kwa kuingia takribani michezo yao mingi, kuchangia pale nilipoweza na kutoa ushauri wa kuisaidia timu lakini NASIKITIKA kusema kuwa juhudi zangu hazijasaidia kwa sababu ambazo nitaziweka baadae humu.
Nakumbuka jinsi nilivyochuma dhambi za UWONGO kwa kudanganya OFISINI kwangu hasa kwa Mabosi zangu kuwa NAUMWA au nina UDHURU ilimradi tu nipate ruhusa niende kutizama mechi za Simba Taifa na hadi Mikoani.
Nina MASIKITIKO makubwa na HASIRA kali sana kwa jinsi timu yangu ya Simba inavyoendeshwa sasa na LEO NAOMBA NITOE MAAMUZI YANGU HAYA MAGUMU KUWA NASITISHA RASMI KUISHABIKIA NA KUJIHUSISHA KWA LOLOTE LILE LINALOIHUSU TIMU YA SIMBA SPORTS CLUB KUTOKANA NA UPUUZI KAMA SIYO UNAFIKI HUU NINAOUWEKA HAPA:
NB: Tumechoka sasa kila kukicha kubatizwa kusikokuwa rasmi kwa kuitwa :
Akhsanteni na naomba kuwasilisha.

- Timu ya Simba kwa sasa INAONGOZWA KIHUNI TUPU.
- Timu ya Simba kwa sasa VIONGOZI WAKE WAKUU Rais na Makamu HAWAPATANI.
- Timu ya Simba kwa sasa IMEKUWA KAMA MBUZI WALIOKOSA MCHUNGAJI.
- Timu ya Simba kwa sasa IMEWEKEZA KATIKA UCHAWI NA MAJUNGU BADALA YA SOKA.
- Timu ya Simba kwa sasa INA WANACHAMA WANAFIKI NA NDUMILAKUWILI.
- Timu ya Simba kwa sasa HAIWAJALI TENA WACHEZAJI WAKE HASA KIMASLAHI.
- Timu ya Simba kwa sasa NDIYO INAZIDI TU KUPOTEZA DIRA KIMAENDELEO.
- Timu ya Simba kwa sasa IMEWEKEZA KATIKA UJINGA NA UPUMBAVU TUPU.
- Timu ya Simba kwa sasa INA LAWAMA NYINGI BADALA YA KUWAJIBIKIA YENYEWE.
- Timu ya Simba kwa sasa INA WIVU WA KITOTO NA USIO NA TIJA KISOKA.
- Timu ya Simba kwa sasa INATAWALIWA NA WANACHAMA WAHUNI NA WASANII TUPU.
- Kufanyike MKUTANO wa DHARURA na timu akabidhiwe Mo Dewji aisuke upya timu.
- Wachezaji wote wa Simba wapewe STAHIKI zao bila vitisho au kudhulumiwa.
- Utaratibu wa timu kuwa chini ya MATAWI yanayoongozwa na Watu WAHUNI, WAONGO na wenye NJAA ukome.
- Makamu wa Rais Kaburu na Mjumbe wa Simba Tully WATUBU kwa Wanasimba kwa kuwa VIBARAKA wa Yanga na kuwa na MAHABA na timu ya Yanga. ( Ushahidi wa haya kuwa Kaburu na Tully ni Yanga damu 100% upo na siku si nyingi nitaweka kila kitu HADHARANI )
- Timu iache kuwekeza sana katika KUFANYA au kupenda USHIRIKINA kuliko kuijenga timu Kisayansi zaidi ili ipate matokeo mazuri.
- Msemaji wa Klabu ya Simba Haji Manara AACHANE NA TABIA YA KILA MARA KUISEMA au KUISHAMBALIA Yanga kwa GHARAMA za UOZO wa Simba wenyewe na badala yake AJIKITE KATIKA KUSEMA UKWELI WA YALE TU YAHUSUYO Simba bila kuwa na UWOGA wowote.
- Rasilimali za Simba ziwanufaishe kwanza Wachezaji na pili MAENDELEO ya Klabu ya Simba.
- Kamati zote zilizoteuliwa ndani ya Klabu ZIVUNJWE RASMI na Kamati ya UTENDAJI tu ya Simba ndiyo IWAJIBIKE katika kuiongoza timu ya Simba.
- Kufanyike UCHUNGUZI wa KINA sana kuweza kujua ni akina nani wapo ndani ya Klabu ya Simba Sports Club lakini WANATOA SIRI ZOTE za Simba kwa WAPINZANI wetu Yanga na bahati nzuri WANAJULIKANA sana.
- Wanachama na Mashabiki wa Simba TUACHE KUWA MAZUZU NA MAJUHA wa KUDANGANYWA kila mara kwa maneno matamu au kauli tamu tamu na TUNARIDHIKA huku timu INAANGAMIA.
- Timu ya Vijana ya Simba B ipewe UMUHIMU MKUBWA SANA na KILA AINA YA MSAADA INAYOITAKA na ikiwezekana iwe chini ya Makocha ambao walikuwa Wachezaji wetu mahiri wa Simba ili waweze kutujengea Kikosi thabiti cha Vijana ambacho kitakuja kutusaidia baadae na hata kutupunguzia gharama zisizo za lazima za kusajili WACHEZAJI MAJIPU wa KIGENI ambao hawana tofauti na Wafanyakazi hewa kutokana na kwamba gharama zao za USAJILI haziendani na aina yao ya Soka kama Wachezaji wa kigeni.
NB: Tumechoka sasa kila kukicha kubatizwa kusikokuwa rasmi kwa kuitwa :
- Wa Mchangani
- Wa Matopeni
- Wa Hapa hapa
- Wa Kunawa lakini asiyekula chakula
- Bingwa wa Kuoa lakini mbovu wa kuzalisha
- Kubwa jinga halafu hovyo
- Baiskeli ya miti
- Simba wa mjini
- Wakurupukaji
- Wa Mabonanza
- Masikini wa akili
Akhsanteni na naomba kuwasilisha.