Nasimama na Spika Ndugai

Watanzania sijui nani katuloga, anatokea mtu anawaambia jamani ee, hapa mnaibiwa, chombo chenu cha kutunga sheria kinayumba, lakini wanatokea watu sijui wana akili gani wanakuwa wanamshambulia tena huyo mtu. Sasa unasimama na spika kwa faida ya nani?

Yaani ni Kama atokee mtu akuambie kuwa mkeo analiwa na jirani afu badala ya kujiridhisha Kama ni kweli au si kweli unaanza kumtukana tena jirani.

Watanzania tumelogwa
 
Uko vizuri bro nimependa ulichoandika... Usikatishwe tamaa na comments ...
Yes Bunge ni dhaifu.... Ila bado ni muhimili usiotakiwa kutukanwa na CAG.....
Endeleni tu kudanganyana CAG ndio hatakiwi kuingiliwa na muhimili wowote kwa sababu yeye ndio mkaguzi wa mihimili yote

Sent using Jamii Forums mobile app
 

CAFG alikuwa akihudhuria mkutano wa dunia wa asasi za ukaguzi wa mahesabu ya serikali na ndipo alihojiwa na waandisjhi wa habari kuhusu taarifa za ukaguzi zilizotolewa na ofisi yake. Tusifikiri kuwa media za wenzetu ni kama hizi za hapa nyumbani zinazokubali kuwekwa kwapani. Asingeweza kusema uongo
 
Ukweli unaweza ukawepo lakini kinachoongelewa hapa ni lugha iliyotumika siyo ya kiungwana. Huwezi kuiita taasisi kubwa kama Bunge eti ni DHAIFU. Lugha hizi tuwaachie wanasiasa wenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app

Waandishi wa habari wa nje sio kama wa hapa kwetu ambao hutayarishiwa maswali ya kuuliza?
 
Usiseme kuwa aliyoyasema CAG bunge hawakuwahi kuyasikia sio kweli wameyasikia na wanayajua kwa sababu report ya CAG ikikamilika huwa inasomwa bungeni

Sasa kama walisomewa report na wakaa kimya uanaka CAG asemeje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chakubanga nimesoma, nimerudia, nimesoma tena bado sijakuelewa🙄🙄
 
Kwani kuna limit ya mahali pa kuongelea kadri ya sheria za nchi?
 
Naunga mkono hoja. CAG awajibishwe kwa maneno na matendo yake. Kukosa staha kwa uaminifu aliyopewa na watanzania kiasi cha kuwadhalilisha namna hii tena huko ng'ambo haiwezi kufumbiwa macho. Awajibishwe. Kumbuka Bunge na serikali vyote vinamilikiwa na watanzania. Kushambulia mmoja wa mihimili ama yote ni sawa sawa na kuwashambulia watanzania. Watanzania hatuwezi kukubali kudhalilishwa na mtu tuliyemuamini na kumkabidhi juku la u-CAG! Tutamuwajibisha kwa taratibu tulizojiwekea kama nchi na tutamsamehe kulingana na taratibu tulizojiwekea pia.
 
Nawewe inaelekea hujamsikiliza CAG alivyosema CAG kajibu swali kua kama bunge halifanyi ... ni udhaifu wa mbunge jifunzeni kusikiliza mtu anapojibu swali na pale anapotoa speech. Halafu unadai kasemea marekani kwa hiyo kaidhalilisha nchi, sasa swali kaulizwa akiwa marekani ulitaka awaambie atalijibu akirudi Tanzania? CAG hana kosa lolote ni uelewa mdogo tu wa watu, Na CAG hajasema bunge ni dhaifu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…