Nasimama na Spika Ndugai


Safi! Umefanya Kazi nzuri na rahisi sana! Wewe ni subjective! Partisan! and Ambitious sycophant!
Hujasumbuka hata kidogo kuhoji mantiki kuu ya CAG!
Ujue Bunge likiendelea kuwa Dhaifu hasara sio ya CAG ni yako wewe kama unalipa kodi! na Watz kama mimi.

CAG hawezi kukurupuka kama wewe ulivyofanya...! Brother kubali tu UMEKURUPUKA! Sio kwamba ni bahati mbaya umerupuka kwa makusudi ya ... na...!!!!!
Wakati mwingine chukua muda wako jiulize unataka kutetea nini? NCHI kwanza vyama baadae!
 
Hoja ya kipuuzi kabisa. Huko nje alienda kama nani? Ikiwa alienda kama CAG basi alikuwa katika wajibu wake, na hivyo hawezi kuhojiwa.

Tinashindwa kumhoji aliyepoteza 1.5 trillion, tunahangaika na mtu anayetuambia ukweli. Very low mind.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wachumia tumbo endeleeni kuungana kutetea dhambi zenu, kiukweli bunge ni dhaifu.Tena halistahili hata kuwepo. CAG kasema alitoa mapendekezo bonge lihoji na mpaka leo limekali ripoti mbali mbali, huu sio udhaifu ni kitu gani?
Kwenda zako hakuna hoja hapo, CAG lazima alindwe kwa nguvu zote
 
Hata kama ananyoosha ukweli, lakini hawezi kuidharirisha Inji popote pale achilia mbali huko ughaibuni.


Tumefundishwa Staha, kuchukuliana, kuheshimiana.
Hata kama kuna shida mahali, tumalizane wenyewe kwa vikao na mijadala ya ndani.

Uzalendo kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawewe njaa imehamia tumboni kwani Bunge si dhaifu??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mburula mwingine wa Lumumba eti CAG ana ajenda ya siri kwa kusema ukweli kwamba tuna bunge UOZO!

Na huyo kichaa jiwe na dhalimu anayechota trillions bila idhini ya Bunge na kukataa uchunguzi huru wa 1.5 trillions iliyopotea ana ajenda ipi?

 
Sijui kinachokusumbua lakini ukae ukijua kuwa CAG ameongea ukweli. Spika angekuwa na busara(bahati mbaya hana) angetoa jibu moja tu, "Hayo ni maoni yake(CAG), sisi tunafanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni tuzizojiwekea". Ila kukosa busara kutalifanya hili jambo liwe kubwa bila sababu za msingi.

Bunge limekuwa dhaifu ni kweli, hilo halina ubishi, mfano mdogo tu; bunge limepewa dhamana ya kupanga mapato na matumizi ya serikali; leo hii Rais anaamua kutumia Bil 600(Tani lakini 2 kwa bei ya 3,000 kwa kilo) kununua korosho. Swali ni je, Bunge lilikaa lini kuamua pesa nyingi kiasi hiki ziende kwenye korosho? Kwanini bunge linapokwa jukumu lake la msingi kabisa, power of the purse halafu liko kimya linacheka tu?
 
Mkuu kwani alichosema CAG ni uongo?
 
Inji iliyojivua nguo nguo unaidhalilishaje?
 
Ulitaka CAG atumie neno gani badala ya neno dhaifu!? Maana ukweli ni kwamba Bunge ni dhaifu, na kama kiongozi wa Bunge naye ni mgonjwa mgonjwa..basi naye ni dhaifu, Bunge kuongozwa na MTU dhaifu ni dhaifu.

Hivyo CAG kuhojiwa na chombo dhaifu, tarajia mahojiani dhaifu, hivyo CAG kuhojiwa na chombo dhaifu inahakisi udhaifu. Uzalendo na udhaifu kamwe haviwezi kukaa pamoja..

Endelea kusimama na Bunge dhaifu, linalotunga sheria za kikokotoo dhaifu, dhidi ya watu au wafanyakazi dhaifu, pamoja na wanaoandaa maandamano dhaifu kupongeza vitu dhaifu

CAG mzalendo anakwamishwa utendaji wake na Bunge dhaifu.. Ahaaa haa haa nimekumbuka upotevu wa 1.5 Trillion dhaifuuuuu


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Uko vizuri bro nimependa ulichoandika... Usikatishwe tamaa na comments ...
Yes Bunge ni dhaifu.... Ila bado ni muhimili usiotakiwa kutukanwa na CAG.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…