baba-mwajuma
JF-Expert Member
- Feb 1, 2014
- 5,472
- 11,035
Cheap propaganda. Wakati huo Persia empire ilikua kubwa Sana ikifika nchi zote za Asia ya Kati mpaka nchi za kiarabu kama Iraq, MTU yoyote alietokea huo Ukanda aliitwa Mpersia hata kama Hatoki Iran ya Leo.Haikuwa Islamic golden age bali ilikuwa Persian Golden age. Uvumbuzi na maarifa yote mnayodai kuwa ni Islamic Golden age yalitokea Persia, Uislam haukuwa na mchango wowote. Jiulizr kwa nini hiyo Islamic Golden age haikuwa na wanasayansi Waarab badala yake karibu wote ni Waajem?
Kwa sasa Wairani wengi wanarudi kwenye asili yao ya Kiajemi (Aryan) na wanachoma Qurani moto.
Wanasema Uislamu haukuleta faida kwa Iran bali uliharibu nchi hiyo.
Watu wengi mashuhuri katika historia ya Kiislamu — kama wanazuoni, wanasayansi, wasanifu majengo na wasanii — walikuwa Wairani wenye asili ya Kizoroasta.
Watu wakubwa kama Avicenna (Ibn Sina) na Al-Khwarizmi walikuwa Wairani.
Usanifu wa majengo ya Kiislamu uliendelea kutoka kwenye usanifu wa Dola ya Sasanian.
Hata sarufi ya Kiarabu, ilipangwa na kuandikwa kwa mpangilio mzuri na Wairani.
Na elimu nyingi za Kiislamu zilistawi mikononi mwa Wairani.
Unaweza jiuliza: kama walikuwa Wairani, kwa nini walikuwa na majina ya Kiarabu?
Jibu ni kwamba katika kipindi cha mwanzo wa utawala wa Kiislamu huko Uajemi watu waliokuwa na majina ya Kiajemi au waliokuwa wakizungumza Kiajemi waliuawa, hivyo walilazimika kutumia Kiarabu ili kuishi. Kipindi hicho huitwa “Miaka Mia Mbili ya Kimya.”
Wairan wanampa heshima ya pekee kwa mwandishi Ferdowsi, anayeonekana kama mlinzi wa lugha ya Kiajemi, kwa sababu aliandika mashairi yaliyosaidia kuhifadhi utambulisho wa taifa lao.
Wanasema kama leo lugha ya Kiajemi bado ipo hai, ni kwa sababu ya juhudi za watu kama yeye.
Mfano kwenye Uisilamu Maimamu wakubwa kama Bukhari actual birth place yake ni Uzbekistan ya Leo ila alitoka Persia ya Zamani, Imam Muslim Actual Birthplace ni Afghanistan ya Leo etc.
Pia hapa Tunaongelea Africa, Spain, Portugal na part ya Ulaya iliokuwa chini ya Uisilamu si Waarabu wa gulf wala si wapersia waliokua hapo Bali ni Moors, kuna scientist kibao toka Huo Ukanda wa Africa waliokua n contribution kubwa na nakutajia na majina na Contribution zao
1. Mohammed Idris ambaye ndio founder wa World map na ramani ya sasa contribution kubwa inatoka kwake, Alitoka Morocco, unaweza UKa Google "Tabula Rogeriana" kuona ramani zake zote.
2. Al-Zarqali (Arzachel) huyu mgunduzi wa saa ya maji, na contribution zake za Astrology mpaka Leo zinatumika, Alipinga Dunia sio Duara bali ni Elliptical amabyo ndio knowledge halisi ya sasa
3. Al zahrawi Baba wa Upasuaji ambaye mpaka Leo anakuwa credited MTU wa Kwanza kufanya Upasuaji wa kisasa, vifaa vyake kama mikasi, tweezers, visu vya Upasuaji Hadi Leo vinatumika Mahospitalini. Huyu jamaa pia mgunduzi wa lipstick na mambo mengine ya urembo pamoja na vitu vya pharmacy kama distillation
4. abass ibn Firnas ambaye ndio mgunduzi wa kifaa cha Kwanza kupaa
5. Kuna Yule bi dada wa Morocco ambaye yupo credited kwa Kuanzisha Chuo cha Kwanza Duniani na kuweka mfumo wetu wa sasa wa vyuo. Etc.
Wasome zaidi hapa.
So si kweli eti Islamic Golden age ilitoka Persia Tu Bali ni sehemu zote, Andalusia ni mfano mzuri kupinga point yako.
Pia ukitoa Hapo kuna Wanasayansi wengi walitoka Uturuki ya sasa, Syria, Iraq, Palestine ya sasa, Egpty etc.