Nashukuru kwa mapokezi niliyopewa NCCR Mageuzi. Kwa namna hii mnastahili kurudi kwenye chati kama chama kikuu cha upinzani

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Siwezi sema ni office gani niliyochukulia kadi lakini kwa ukweli nimeamini ile Slogan yenu ya Udugu mnaitekeleza.

Nimekuja kuchukua kadi nimelipia ada za mwaka mzima. Mmenipokea vizuri sana. Mmeonesha ukarimu wa hali ya juu.
Kwanza ofisini nimepewa heshima kubwa sana.

Pia mmenipatia mikakati mizuri sana ambayo kwa sasa ni siri yangu sababu kuna jimbo mtanipitisha nigombee lakini naiweka kama siri yangu.

Pia nimefurahi sababu mnatambua juhudi za Mh JPM za kupambana na ufisadi na kutekeleza miradi mikubwa katika utekelezaji wa ilani ya chama chake. Pia nashukuru kwa lunch la nguvu ambalo tulikula kwa pamoja na kutiana moyo.

Hivyo tusubili October ifike ili matakwa yetu yatimie.

Siasa si uadui. Tuwe wazalendo.
 
Hilo ndilo sharti alilopewa Mbatia ili aweze kugawiwa majimbo kama Mrema. Ila hawatofanikiwa.
Anajulikana vunjo pekee,
Wameshindwa polisi,tiss,wasiojulikana, manunuzi,DPP ,msajili kuuwa upinzani Ndio yeye ataweza? Yeye alambe tu ruzuku bahati haiji mara mbili zimfae uzeeni
 
Nakumbuka uchaguzi ule wa mwaka 1995, nikiwa mwaka wa mwisho "under graduate program" ambapo nilikuwa miongoni wa wanachuo ambao tulimsikiliza Mh. Lyatanga Mrema pale Nkurumah Hall akiwa mpeperusha bendera wa nafasi ya uraisi huku akinadi sera za NCCR Mageuzi, na hatimaye kulisukuma gari mpaka geti la UDSM lenye kupakana na Chuo cha Maji, kuelekea njia ya Ubungo.

Nakumbuka, nilikuwa ni mmojawapo wa mawakala ambao tuliteuliwa na chama hiki, ijapokuwa hatukuwa ni wanachama, bali sifa zetu tulikuwa ni wanachuo wenye misimamo thabiti ya kutaka mageuzi. Tullifanikisha kwa ukamilifu zoezi hili ambapo Marehemu Masumbuko Lamwai akaibuka mshindi ktk nafasi ya ubunge.

Pamoja na kuwa ktk kipindi cha mitihani ya kitivo, enzi hizo hatukuwa na mambo ya "collage" chama hili kilitupekeka chaka. Kwa hisia zangu sina imani ya chama hiki chenye "elements" zote za kishushu. Hiki kwa hakika ni "CCM B" toka kwa asili yake na waasisi wake. Wenye kukishabikia na kukumbatia mnalo, hakiaminiki wala kutegemewa kama chama chenye nia ya dhati kuwa "icon of excellence" kwa nia ya kushika dola.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kuchafua chama cha wazalendo kama umetumwa waambie waliokutuma sisi sio mamluki.
 
Back
Top Bottom