Nashindwa kumtofautisha Shibuda na popo!

Nashindwa kumtofautisha Shibuda na popo!

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,167
Reaction score
162,602
Moja ya viumbe wa ajabu duniani ni huyu aitawe popo.Kiumbe huyu hajulikani yuko kundi gani,kama ni mnyama au ndege.

Hali kadhalika,mh.Shibuda leo nae amethibitisha kuwa haeleweki yuko kundi gani, kama ni la wapinzani au bado ni mwana ccm.

Jioni ya leo, akichangia hoja bungeni, mh.Shibuda alionekana kutumia muda wake mwingi kulalamikia namna bunge linavyoendeshwa kiasi cha kumfanya mwenyekiti wa bunge, mh.Hassan Zungu, mbunge wa Ilala, kumkatisha na kumtaka achangie hoja iliyokuwa mezani na si kuendelea kulalamika na kulaumu..Amediriki kusema bunge linatakiwa kuhakikisha hata wale walio wachache ndani ya bunge wanaheshimiwa na kusikilizwa.Mh.Shibuda alionekana wazi kulaani namna hoja binafsi za wabunge wa upinzani zilivyopokelewa na kushugulikiwa.

Sasa wakuu tukirudi nyuma,huyu mh.Shibuda sio ndio huwa mara kwa mara hutumia vikao vya bunge kuwalaumu na kuwaponda wapinzani huku akishangiliwa na wabunge wa ccm!Ni mara ngapi ametumia vikao vya bunge kukiponda chama chake kwa mafumbo huku wabunge wa ccm wakimshangilia?Swali ni je huyu bwana huwa anasukumwa na uadilifu au personal interest zake pala anapotoa mawazo yake ndani na nje ya bunge?Hivi leo hii ndio kagundua uovu wa ccm na serikali yake?Au magamba wamemgeuka?

Je ni kundi gani ambalo huyu bwana anastahili kuwekwa?
 
Kwa ushahidi wa kimazingira uliopo na unaoonekana hadi sasa ni kwamba huyu mtu anatumiwa na hivyo ndivyo anavyotumika, yaani anang'ata sana na kupuliza kidogo, wewe humuelewi yuko wapi lakini waliomtuma wanamuelewa vizuri wenzio, hapo anasubiri payrol yake tu isome, nayo hiyo ni sehem ya kazi yake, msubiri tena mda mfupi ujao utamsikia.....Ndio siasa hizo.
 
Back
Top Bottom