Nashindwa kuamini kinachoendelea bongo

mululu

JF-Expert Member
Nov 7, 2014
749
406
Wengi wamesema juu ya watu kushabikia mambo bila kufikri kiundani wanachoshabikia, nami nimeona ninene ya moyoni.

Juzi nilikuwa nasoma makala moja ktk gazeti la Raia mwema iliyoandikwa na bwana Lula Wandali Mwananzela iliyoenda kwa title " Magufuli kiongozi bora kuwahi kutokea tz" Muandishi huyu alikuwa mtu makini sana kipindi cha nyuma lakini sijuwi naye kaingia lini kwenye kundi la kusaka u DC??

Jamani hv ni kweli tumeshakubali utendaji hata kufikia kusema hajawahi kutokea mtu bora zaidi yake?? Mimi nadhani uongozi bora utapimwa kwa kuangalia ubora wa maisha ya walala hoi, tujiulize tuu hv ni kweli maskini tupo na AHUWENI kwa sasa ambayo haijawahi kutokea????

Mambo makubwa kama mikataba mibovu kavunja mingapi mpaka sasa?? Na yanayofanana na hayo.

Ukiacha suala la sukari, je mkulima mpaka sasa jee mazao yake yanamlipa zaidi ya kipindi kingne chochotee??

Jee rais bora kuwahi kutokea hp tanzania afiche bunge kwa manufaa ya nani??

Haka kapicha ninakokaona mm naamini na wengne watakaona baadae
 
Sasa wewe ndugu, si ungethibitisha vinginevyo makala ya Lula kwa kuonesha takwimu kinzani dhidi ya makala yake badala ya kuuliza maswali na hisia za kisiasa? Lakini pia siyo jambo jema kudhani kila anayeunga mkono juhudi za awali za Rais Magufuli anatafuta U-DC. La hasha. Kuna watu wataalam kabisa wanaochambua mwanzo wa approach ya JPM waka-project coclusions za kitaalam pia. Kwamba kuna mafanikio huko taifa liendako. tafadhali ukitaka kuheshimika acha ku-generalise.
 
Mkuu kwani hujui bwana Lula Wandali Mwananzela anatokea wapi Tanzania??? lazima tumpambe wakwetu
 
Sasa wewe ndugu, si ungethibitisha vinginevyo makala ya Lula kwa kuonesha takwimu kinzani dhidi ya mkala yake badala ya kuuliza maswali na hisia za kisiasa? Lakini pia siyo vjambo jema kudhani kila anayeunga mkono juhudi za awali za Rais Magufuli anatafuta U-DC. La hasha. Kuna watu wataalam kabisa wanaochambua mwanzo wa approach ya JPM waka-project coclusions za kitaalam pia. Kwamba kuna mafanikio huko taifa liendako. tafadhali ukitaka kuheshimika acha ku-generalise.
Watanzania tujifunze kuwa na mtazamo mpana wa mambo mbalimbali ya nchi yetu badala ya kuwa na mihemuko ya kiitikadi (ushabiki) wa kivyama(Kisiasa) au mtazamo wa kibaguzi wa aina yoyote ile,si vibaya kumkosoa JPM kwenye mambo yenye mamtiki,lakini ni vema kuweka mizania au kupima yale ambayo yanafanyika ktk serikali yake sasa na impact yake hapo siku za baadae,baadhi yetu wa Tz tumeanza kulalamika na kushutumu baadhi ya hatua hizo za Rais,bila kujua ya kwamba mambo mengi mazuri tunayo yatarajia,hayawezi kupatikana bila ya hatua hizo mathubuti kuchukuliwa sasa,pia muda wa JPM toka alipochukua nchi ni mfupi sanaa kiasi cha kumshutumu,hivi ni kweli yaliyofanyika chini ya serikali yake mpaka sasa hayana dhamira njema kwa mustakabari wa nchi yetu siku zijazo?tuweke siasa kando,tutafakari kwa kina kwa faida ya wananchi wote na si kwa maslahi ya watu wachache.
 
Si mlisema rais anatekeleza sera za ukawa!!! Sasa unaandika utumbo gani
 
Wengi wamesema juu ya watu kushabikia mambo bila kufikri kiundani wanachoshabikia, nami nimeona ninene ya moyoni.

Juzi nilikuwa nasoma makala moja ktk gazeti la Raia mwema iliyoandikwa na bwana Lula Wandali Mwananzela iliyoenda kwa title " Magufuli kiongozi bora kuwahi kutokea tz" Muandishi huyu alikuwa mtu makini sana kipindi cha nyuma lakini sijuwi naye kaingia lini kwenye kundi la kusaka u DC??

Jamani hv ni kweli tumeshakubali utendaji hata kufikia kusema hajawahi kutokea mtu bora zaidi yake?? Mimi nadhani uongozi bora utapimwa kwa kuangalia ubora wa maisha ya walala hoi, tujiulize tuu hv ni kweli maskini tupo na AHUWENI kwa sasa ambayo haijawahi kutokea????

Mambo makubwa kama mikataba mibovu kavunja mingapi mpaka sasa?? Na yanayofanana na hayo.

Ukiacha suala la sukari, je mkulima mpaka sasa jee mazao yake yanamlipa zaidi ya kipindi kingne chochotee??

Jee rais bora kuwahi kutokea hp tanzania afiche bunge kwa manufaa ya nani??

Haka kapicha ninakokaona mm naamini na wengne watakaona baadae
Simple mind discuss people Great mind discuss Issues . Sasa watu wengi hawawezi kumwelewa`Magu
 
Mabadiliko na juhudi za wazi anazofanya Rais Magufuli katika kuongoza nchi bado haziwezi kumthibitisha kuwa kiongozi bora zaidi kuwahi kutokea. Unahitajika muda na vigezo kuzingatiwa.
Hizi za sasa ni sifa za kijuha tu hata anayesifiwa analijua hilo.
 
Tuheshimu pia mashaka waliyonayo wengine. Hizi "rhetoric" hata mimi sikuabaliani nazo. Wote tunampa support JPM na tunaona na kukubali kazi anayofanya. Tuendelee kuamini hivyo bila kuongeza vionjo na chumvi (Chaguo la Mungu, Hajawahi kutokea, Zawadi toka kwa Mungu, Rais bora Afrika, nk). Tusikimbilie sana kusema hayo "maneno ya mwisho" kama mwanamuziki mmoja alivyowahi kuonya, kwani hayana maana sana, ni mbwembwe tu na si lazima ziwe sifa zake za uongozi. Tukilazimisha kumpa mbwembwe hizi, hapo baadaye tutataka kumdai kulingana na matarajio yetu hayo makubwa kupita kiasi.
 
Wengi hawajanielewa nimeandika nini, nimeuliza jee ni halali kusema Magu ndiye mtu bora kuwahi kuongoza taifa hili?? Pia nikaulza harakati zake n kwa namna gani zinabadili maisha ya washangiliaji wake??
 
Ni kweli hajawahi tokea rais anaekamata mifuko semanini ya sukari na kuifanya habari kuu ya taifa huku nchi ikiwa na uhitaji wa tani laki nne kwa wakati huo huo.
 
H umenifurahisha sana mkuu
 
Kuna Mdada kwasasa anajiita GIGY Money, kuna Wema Sepetu wote hawa ni wasaka kiki kwa nguvu !!

Ukweli ni kua JPM anajitahidi sana kutaka kuikomboa Tz, tatizo kubwa la JPM ni kutaka kufika anapotaka ila hajui njia ipi sahihi ya kumfikisha atakapo. Nakiri dhahiri kua amekua akikurupuka sasa, nkimanisha kua anaona kile aamuacho ndicho sahihi na hakuna wa kumkosoa.

Sasahv wakuu wa taasisi mbalimbali nchini wanafanya kazi siyo kwa kuzingatia taaluma tena ila kwa influence ya kumfurahisha mkuu wa nchi, kitu ambacho kinarud kuwakandamiza wananchi.
Wengi hawajanielewa nimeandika nini, nimeuliza jee ni halali kusema Magu ndiye mtu bora kuwahi kuongoza taifa hili?? Pia nikaulza harakati zake n kwa namna gani zinabadili maisha ya washangiliaji wake??
 
Simple mind discuss people Great mind discuss Issues . Sasa watu wengi hawawezi kumwelewa`Magu
Mkuu acha kukariri vimisemo ambavyo havina uwiano na uzi lengwa. Mjibu kwa hoja. Rais ni taasisi siyo a single person kwa kuangalia tu. Je ameshakidhi dukuku za Watanzania kiviiiiileee? Panda juu ya mlima mizeituni na uangalie pale Yeriko watu wana matumaini?
 
Wengi hawajanielewa nimeandika nini, nimeuliza jee ni halali kusema Magu ndiye mtu bora kuwahi kuongoza taifa hili?? Pia nikaulza harakati zake n kwa namna gani zinabadili maisha ya washangiliaji wake??
Ngoja nikujibu mm niliye kuelewa kwanza siyo halili kusema magu ndiyo rais bora kuongoza taifa ili kwanza ata mwaka tu ajamaliza akuna ahadi aliyoaidi ata moja iliyo tekelezwa na ikaisha na pia maisha mtaani ni magumu sana pesa akuna ajira akuna katika kipindi kifupi cha madaraka yake tumeshuudia watu wengi wakikosa ajira kwa kifupi tusubiri miaka mitano
 
Back
Top Bottom