Nashauri waziri Magufuli ashtakiwe


Mkuu pamoja na hoja zako nyingi lakini naona jazba imelitawala bandiko lako. Huenda ni kweli Magufuli alifanya siasa lakini yeye si mwanasheria. Sifahamu kama unajua mchakato wa kumshitaki mtu hasa kwenye makosa ya jinai.

Katika hili mimi nilitegemea lawama kubwa ingetupwa kwa DPP kwa sababu ndiye aliyekubali shauri hilo liende mahakamani na ndiye huyo huyo aliyetoa nolle prosequi hii ambayo imewaachia huru wachina. Hii hati mara nyingi hutolewa baada ya kuona ya kwamba huna ushahidi wa kutosha kuendelea na kesi.

Je wakati DPP anaipeleka kesi mahakamani hapo awali na serikali ikashindwa hakuangalia ushahidi kabla ya kuchukua uamuzi? Kama Magufuli alifanya siasa, je na DPP naye aliingia katika siasa na kuacha sheria?

Naona unamuonea bure Magufuli kwa kusema ati aliwapeleka wachina mahakamani! Magufuli hana uwezo kisheria kuwapeleka watuhumiwa wa jinai mahakamani hata kama angependa waende mahakamani lazima ruhusa itolewe na DPP baada ya kutathimini ushahidi wa shitaka husika.

DPP alitoa ruhusa kesi ikaenda mahakamani, prosecution side ikashindwa kutoa ushahidi pasipo na shaka kuishawishi mahakama kuwatia hatiani wahusika. Kisha huyo huyo DPP anatoa Nolle Prosequi kwamba haendelei na kesi!!

Hukuwafaidi samaki!!!!?
 

Naunga mkono hoja yako juu ya kupotea kwa meli. Hata kama tungeshinda kesi, meli yao iko wapi?? Kwanini izame? Wanaodai ilipigwa dili na viongozi serikalini kisha wakaizamisha tuwaamini?? Je hii si hujuma?
 
RAISI Wa nchi hii anawaogopa wateule wake hana maamuzi magumu hata tyson wasira anampinga kukutana na ukawa
 
kuhusu rizwani kushikwa china, mimi sio msukule. nenda kawadanganye misukule wenzio.
 

Hayo ni mawazo yako tu, naomba ufahamu kuwa Dr. Magufuli angefaa kushitakiwa endapo wale wachina wangeachiwa palepale baada ya kupelekwa mahakamani lakini mahakama iliwaona wana hatia na ikawafunga liko wapi kosa la magufuli? Na ni mahakama hiyohiyob ndiyo imewachia huru Hakimu aliyewafunga ndiyo ashitakiwe na siyo Magufuli, halafu Hati ya Nole hutolewa na mlalamikaji yaani serikali sasa kama ni serikali inawaachia kutokana na sababu zake binafsi au kwa kuongea nchi wanakotoka wafungwa hao Magufuli kahusikaje hapo, lakini kumbuka rushwa inatembea kuliko unavyoelewa.
 

Na kuna watu wanapenda eti Magufuli huyu huyu awe rais!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…