magode
JF-Expert Member
- Oct 2, 2014
- 2,204
- 3,338
Salaam wana MMU,
Vyeti vya ndoa vinavyotolewa makanisani,misikitini na bomani vyote ni mali ya serikali. Nimejaribu kutafakari jinsi ndoa zinavyokuwa ngumu kila kukicha,kuna watu wanaishi maisha ya mateso sana katika ndoa zao kwa kuheshimu hivyo vyeti wakiamini ni kumkosea Mungu kana kwamba hivyo vyeti ni mali ya Mungu.
Kuepusha madhira yanayoendelea katika ndoa,napendekeza vile vyeti viwe na kipindi cha ukomo ili kuwaokoa watu wengi wanaoona aibu kujitoa katika kifungo cha ndoa.
Wanandoa wakifunga ndoa,wapewe miaka 5 ya matazamio kama mmoja wao katika hiyo miaka 5 atakuwa hajaridhika,anaondoka bila kelele. Kama kila mmoja atakuwa amefurahia maisha,utaratibu utawekwa wa kuongezewa muda.
Huu ni mtizamo wangu kutokana na kile nnachokiona katika jamii. Unaweza kuniona km mpuuzi hapa kwa kuandika haya,lakini yakikukuta utatamani ukiangalie cheti chenu kama kina expire date.
Nawasilisha.