apolycaripto
JF-Expert Member
- Feb 11, 2011
- 644
- 225
Kwanza naomba kutamka wazi kuwa Rais wetu pendwa, pasipo kutarajia amejikuta ndani ya mgogoro wa kikatiba katika teuzi zake. Ni kweli Mkuu wetu amevunja katiba ama yuko katika tishio la kuvunja katiba, na hili halina ubishi kwani ibara ya 66.- (1) (e) iko wazi na haina utata wowote.
Kinachosikitisha mpaka kuomba mjadala huu ufungwe, ni kutokana na wasomi wetu bobezi katika fani ya sheria, kutumia weledi wao kupotosha tafsiri halisi ya ibara hii bila kujali maslahi mapana ya Uongozi unaojali misingi ya katiba hasa katika siku za usoni.
Kumekuwa na kauli nyingi tu za kutaka kulaghai umma kuwa katiba haijavunjwa ama hakuna tishio la kuivunja katiba (kwa maana ya kuwa wabunge wawili wa jinsia moja bado hawajaapishwa ama kujiuzulu kwa mmoja wa wateule wa Mkuu). Ukweli ni kuwa iwapo Wabunge hawa wataapishwa kwa kisingizio kuwa Dr. Possi ameachia nafasi, lipo tishio la baadae kwa Viongozi kuvunja katiba wazi wazi kwa tafsiri ya ujanja ujanja kama hii iliyojitokeza.
Katiba kama sheria MAMA haikupaswa kuwa na tafsiri ngumu kama ambavyo baadhi ya wasomi bobezi katika sheria wanajaribu kutuaminisha. Hivyo basi kwakuwa katiba si msingi wa maendeleo ya Taifa letu kwa sasa (haina athari ikivunjwa) , tukubali tu kuwa KATIBA HAIJAVUNJWA na MHE. RAIS YUKO SAWA. Hii inathibitishwa na Mhimili mmoja (BUNGE) kujaribu kutengeneza mazingira ya kupingana na hoja hii.
Katika kuomba kufungwa kwa mjadala huu, naomba kuweka changamoto hapa kupitia mmoja kati ya wanaJF mwenzetu, ambae ametoa ufafanuzi huu kwa maana ya kupata mantiki tu ya nini maana ya sheria ya zuio katika teuzi:
" Mfano uteuzi wa wabunge 10 ukishakamilika na bahati mbaya au nzuri mmoja akafariki, ina maana nafasi moja itarudi kuwa wazi tena na Rais anaweza kiteua mwingine kujaza nafasi hiyo tena?
Nauliza hivi kwa sababu nielewavyo mimi uteuzi wa hizi nafasi ni sawa na zile nafasi 3 za substution ktk mchezo wa mpira wa miguu (football)
Kwamba kocha ukishafanya sub ktk nafasi zako zile 3 na bahati mbaya mchezaji mmoja akaumia na akawa hana uwezo wa kuendelea na mchezo na muda wa mchezo ukiwa bado haujakwisha, ni wazi utalazimika kumaliza na wachezaji 10 uwanjani kwa sbb utakuwa umemaliza nafasi zako kisheria!!
Nadhani hata kwa Possi ili mradi alikwishaga apishwa kuwa mbunge, ni wazi rais alishaitumia nafasi yake hiyo and it is absolutely irreversible hata kama Possi atakuwa amekosa sifa za kuwa mbunge kwa mujibu wa katiba...!!"