Watanzania tumekuwa na utamaduni wa kiimani kwa dini zote zilizopo hapa Tanzania kuombeana na kutakiana mema hili ni jambo zuri sana. Tunapokuwa na matatizo tunaomba na kuombeana sawa. Imani hizo zinajengeka na kutumaini dua ziweze kumbadilisha ALIYEOMBEWA KUONDOKANA NA HALI FULANI NA KUBADILIKA. Kama anayeombewa ana matatizo tunamuombea tukiamini matatizo yataondoka na kupata ahueni.
Nasikitika kwa yanayompata rais magufuli, huyu ni kiongozi anayeongoza kwa kuombewa na kutaka watu wamuombee. Tumemuombea sana lakini hakuna mabadiliko na anayoyafanya NI ZAIDI YA YALE YALIYOPITA.
KWANZA LUGHA KWAKE IMEKUWA TATIZO KUBWA, KUTOKUJUWA WAPI ATUMIE LUGHA IPI NA KWA VIPI ITALETA ATHARI GANI?. Ni mara ngapi Rais hulalamikiwa kwa lugha zake zisizofaa kwa muktadha wa tukio na eneo ?
Kwa mfano kulikuwa na haja gani ya kutumia maneno ya fyoko fyoko kule Zanzibar katikati ya sintofahamu ya uchaguzi wa 2015?
Kulikuwa na haja gani kuwaambia wahanga wa njaa kwamba asiyefanya kazi na asile ?
Mifano ni mingi lakini haitoshi tunamuombea busara na hekima lakini habadiliki. Sasa ametwambia tumuombee uraisi usimtie kiburi. Kumbe anajuwa kuwa ana kiburi?
Watanzania wangapi wameathirika ama na maamuzi au kauli za rais magufuli ? Hata kama ana nia njema kwa kweli lakini kuna kitu anakikosa "busara na hekima "
LABDA TUMUAPIZE.
Maapizo huwa ni kama kukusudia jambo limtokee mtu kwa nia ya baada ya kushindwa njia nyengine . Hapa nakusudia kuwa kwa kumuombea bado haijafua dafu labda tujaribu kumuapiza awe na busara na hekima pengine mungu anaweza kutupokelea maombi yetu.
Tumuapize aache kiburi na awe na busara ya mambo. Maapizo yanaweza yakasibu kubadilisha jambo sugu. Rais wetu maombi kwake yamekuwa sugu kumbadilisha na ndio nikashauri labda tumuapize.
Kishada.