NASA yaghairi kumuapisha Raila Odinga..

Travic

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
720
1,000
Wameufyata?

Upinzani nchini Kenya wamesema baada ya mashauriano na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Kenya, wameona wasitishe shughuli yao ya kumuapisha Kiongozi wao Raila Odinga..

Watamuapisha sambamba na uzinduzi wa bunge la wananchi huko baadae katika tarehe mpya itakayotangazwa muda wowote..

Hivi karibuni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali nchini Kenya alitahadharisha uamuzi wa NASA kutaka kumuapisha Odinga kinyume na utaratibu na kusema endapo watafanya hivyo basi watashitakiwa kwa uhaini..
-------------

Kutoka BBC Swahili;

Shughuli ya kumuapisha Odinga kama rais wa Kenya imehairishwa

Muungano mkuu wa upinzani nchini Kenya NASA, umetangaza kuhairishwa kwa shughuli ya kumuapisha kinara mkuu wa muungano huo Raila Odinga na Stephen Kalonzo Musyoka, kama rais na makamu wa rais mtawalia wa Jamhuri ya Kenya, kwenye Shughuli ambayo ilikuwa imepangwa kuandaliwa tarehe 12 mwezi huu.

Katika taarifa iliyotolewa leo na muungano wa NASA ni kuwa tarehe mpya ya kuapishwa kwa Bw. Odinga na Musyoka, na pia kuzinduliwa kwa mabunge ya wananchi itatangazwa baadaye.
 

Prince leonny

Senior Member
Aug 31, 2017
102
225
Mhuuuuuuh yale yale bongo tunaahirisha ukuta ni sikukuu ya wanajeshi ukishindwa sema bhana ee kabali imeniingia acha nyoya tukutane 2022 hapo
 

Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
9,900
2,000
Kujaribu kumuapisha Odinga ni upumbavu uliopitiliza. Kenyatta awashughulikie tu wakitenda uhaini huo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom