Narudia kuangalia season ya Merlin. Aisee Guenevere alikuwa penda penda mno ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Attelan

JF-Expert Member
Oct 12, 2023
434
701
Gwala wana Jeifu!

Baada ya kupita miaka kadhaa nimeona niirudie hii season ya Merlin. Kwasasa nipo Season 2 episode ya 4.

Tangu imeanza nikiwa naitazama kwa juu nimegundua kwamba uhusika wa Guenevere uliwekwa kuwaonesha wanawake wasio na msimamo kwenye mahusiano. Siku ya kwanza Guene alipokutana na Merlin alikuwa akikenua ovyo ovyo na alitokea kumkubali ila haijulikani alimuweka wapi ila alifurahi kukutana na Merlin na kuongea nae.

Scene ya kwanza niligundua pale alipokuwa akiongea na Merlin baada ya Merlin kuongea maneno ya kejeli kwa Arthur Pentdragon nakumuita mjinga (Prat). Guene alisema amependa Merlin alivyomchallenge Arthur.

Baada ya muda Merlin alipewa adhabu ya kurushiwa matunda yaloyooza na hapo alikutana tena na Guene ambaye aliishia kuwamwagia sifa wanaume wenye misuli na miili iliyojengeka. Na mfano akautoa kwa Arthur. Hapa alipinduka na kuamia kwa Arthur.

Episode nyingine ambayo mwanamke mchawi ambaye mtoto wake wakiume aliuliwa na Arthur na yeye kuahidi kulipiza kisasi alienda porini na kumuua muimbaji aliyepangwa kutumbuiza na hapo kabla ya sherehe Guene alianza kumwagia Morgana sifa mbele ya Merlin na baada ya muda alidahi anapenda wanaume kama Merlin.. "not exactly YOU, but I like men like YOU" (Si wewe, ila napenda wanaume kama wewe).

Siku zilisonga hatimaye episode nyingine alitokea Lancelot yule aliyefoji utambulisho wake na kujidahi yeye ni mtoto wa kishua, mastamaindi alikuwa Merlin. Guene alionesha tena kumpenda Lancelot. Lakini huyo huyo Guene anashare kiss na Arthur kwa mara ya kwanza pale ambapo Arthur anataka aprove mbele ya watu kwamba ana uwezo wa kupambana na anaamua kumtafuta mtu atakayekuwa akionekana wakati wa kutambulisha wapambanaji huku yeye akiingia kwenye mapigano.


Kama Guene angekutana na Myro inawezekana angempenda kabisa. Modred alikuwa na umri mdogo ila nae angependwa na Guenevere ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Duh kwel muda
Nakumbuka hio ilikua ikitoka bbc jumatano tunashinda nkurumah kudowload kwa free wifi kipande kimoj kimoj
 
Back
Top Bottom