NARC iliwadanganya wakenya-Kinana

NARC iliwadanganya wakenya-Kinana

meningitis

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Posts
8,464
Reaction score
4,828
Ni bahati mbaya sana kwa kuwa hatuna utaratibu wakusikiliza kwa umakini na kuchambua hotuba zinazotolewa na viongozi mbalimbali wa kisiasa nchini hasa wanapokua kwenye mikutano yao ya kujenga vyama.

Bahati nzuri mimi nilijitahidi kumsikiliza kinana hiyo juzi na moja ya maneno aliyotamka ni kuhusu chama cha muungano wa NARC cha nchini kenya.

Kinana alikuwa akiifananisha ahadi ya chadema ya katiba ndani ya siku mia moja na ahadi ya NARC enzi hizo,alisema NARC iliwaahidi wakenya katiba mpya ndani ya muda mfupi lakini katiba ilipatikana baadae sana tena karibia na uchaguzi mkuu.

Baada ya kutamka haya ndg Kinana kama anavyopenda kuitwa alisititiza ''hata wakichukia(hao NARC) acha wachukie''

Hapa naona Kinana alimrushia dongo babu Kibaki ambaye juzi juzi tu tumempatia barabara ya bwagamoyo!
 
Meningiatis,Hizo ndio siasa za nchi yetu ambapo viongozi wetu wanalinganisha mambo ya nchi yetu na nchi ambazo ziko mbali nasi kimaendeleo yaani mlima na kichuguu.

Mimi na wewe tutaelewa anachosema lakinimwananchi wa kijijini hata TV hakuna ataelewa alichomaanisha? Wananchi wa vijijini hata wanajua nini NARC?

Viongozi wwetu wamelewa madaraka na kukaa katika ofisi za viyoyozi lakini hawajui wananchi vijijini wanaishi maisha ya namna gani.Ndio maana ulinganifu wao wa vitu hauakisi maisha ya wanaowatolea ulinganifu.
 
Sikumbuki kusikia Chadema au Dr. Slaa au Mbowe wakisema watatoa katiba ndani ya siku100. Najua walichosema ni kuwa wataanzisha mchakato wa kupata Katiba mpya ndani ya siku 100.

Sasa kama wao wanajua ugumu uliopo katika kuandaa katiba na baada ya kujifnza kutokana na uzoefu wa Kenya; kwa nini wanataka kutupatia katia ndani ya miaka 2?

Uchaguzi wa mabaraza ya katiba ni bomu na bado tunasema kuwa tuko sawasawa. Huyu ndo mzee wa meno ya tembo!
 
Huo ulikuwa ni ujumbe maridhawa kwa wale wote wanaodhani Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikitoka madarakani nchi nzima wananchi watakuwa wanapitishiwa maziwa fresh kila asubuhi.
 
Meningiatis,Hizo ndio siasa za nchi yetu ambapo viongozi wetu wanalinganisha mambo ya nchi yetu na nchi ambazo ziko mbali nasi kimaendeleo yaani mlima na kichuguu.Mimi na wewe tutaelewa anachosema lakinimwananchi wa kijijini hata TV hakuna ataelewa alichomaanisha? Wananchi wa vijijini hata wanajua nini NARC? Viongozi wwetu wamelewa madaraka na kukaa katika ofisi za viyoyozi lakini hawajui wananchi vijijini wanaishi maisha ya namna gani.Ndio maana ulinganifu wao wa vitu hauakisi maisha ya wanaowatolea ulinganifu.

Hiyo ndiyo CCM bana. Kumbukumbu mkichwa ni ZIRO!!
 
Alafu hizi siasa za ku compare na kutaja taja vyama vya siasa vya nchi jirani inapendeza kweli.?juzi nilimuona nape akimponda odinga..kinana nae akaja na yake..hivi hawana mifano ya kuongelea hawa watu.?hivi ccm wamekosa sera mpaka inabidi wachanganye na mambo ya kwa jirani? Heshima ya kidplomasia iko wapi?

Kwanza serikali ya narc ilifanya maendeleo makubwa sana,chini ya odinga akiwa waziri wa ujenzi walijenga highways nyingi sana..pia vugu vugu la mabadiliko ya katiba yalianzia hapo.

Sasa kinana na nape wanafanya siasa za karne ipi jamani..hu sio ufinyu wa kujenga hoja kweli? Au wameishiwa?
 
Mtu anahutubia huku anawaza tembo wanaohamia Kenya, kwa nini asiwaponde wakenya?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom