Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakimkosoa Raisi Magufuli kwa yale anayoyafanya na kumtaka kwanza ajenge huwo wanaouita mfumo utakaoweza kujiendesha, wengine kama Kitila Mkumbo ambaye ndiyo muumini mkubwa wa hili neno Mifumo na siku zote humnukuu Raisi Obama alivyosema Ghana kwamba ,,Afrika does not need strong men, but it needs strong institutions"!
Sasa basi binafsi siamini kwamba tatizo letu kama TanZania ni kukosekana kwa mfumo, bali tatizo letu kubwa ni Umaskini na hali duni ya Maisha inayosababishwa na kipato kidogo cha MtanZania, hivyo maadamu hili tatizo hatujalishughulikia hakuna kitakachobadilika hata ujenge mfumo gani!
Hivyo anavyofanya raisi Magufuli ni sawa kabisa kwanza ni lazima aongoze kwa mkono wa Chuma ili kujenga Uchumi wetu kwanza ambao ni Imara ambapo itapelekea pato letu kuongezeka baada ya pato letu kuongezeka sasa mambo ya Mifumo mnayoiongelea itajitatua yenyewe, kwa maana ikumbukwe kwamba watu wanaoiba au kula rushwa TZ siyo kwamba ni watu wabaya au wana DNA ya rushwa HAPANA, wengi wao ni kwa sababu mishahara yao haiwatoshi kujikimu, kwa mshahara wa MTZ wa kawaida inasemekana unaisha baada ya wiki mbili tu, sasa hizo wiki mbili zilizobakia ataishije?
Na hata hawa wanaolalamikia mifumo pia nao ktk kazi zao kama hawafanyi kazi kwenye mashirika ya Kimataifa na wako Serikalini ni lazima hata wao kuna mahali wanachukuwa fedha au huduma isivyo halali ili kufidia pato lao!
Ndio maana kuanzia trafiki, Mwalimu shuleni, Nesi au Daktari Hospitalini wanajaribu kwa kutumia nafasi zao kuchukuwa rushwa au huduma isivyo halali ili kuweza kufidia hizi wiki mbili zilizobakia, hivyo hakuna mfumo ambao unaweza kuondoa rushwa na ufisadi TZ bila ya kwanza kuongeza kipato cha MtanZania, yaani lazima kwanza MtanZania aweze kuishi kwa mshahara wake yeye pmj na familia yake!
Na raisi Magufuli analijua hili kwa maana ni Intelligent man na ndiyo maana amesema ,,atakayetukwamisha tutambomoa", kwani mifumo haiwezi kufanya kazi kama mishahara wa wananchi haitoshi hata chakula tu achilia mbali mambo mengine, hivyo Uchumi kwanza na hili kwa mazingira yetu linawezekana tu kwa kuwa na Kiongozi mwenye madaraka makubwa kupitiliza ili aongoze na kuchukuwa maamuzi magumu na ya lazima haraka na mara moja hiyo ndiyo njia pekee na baada ya hapo sasa hiyo mifumo itajiendesha tu kwa maana mtu aliyeshiba, ambaye watoto wake wameshiba, wanakwenda shule, na pia wanapata mahitaji yote muhimu kwa hali ya kawaida hana haja ya kuiba na siyo kinyume chake!
It's economy, stupid!