Napendekeza motion hizi zifutwe

Napendekeza motion hizi zifutwe

Cybercurex

Member
Joined
Jan 19, 2023
Posts
98
Reaction score
238
Tunaamini na tunafahamu lengo la debate ni kuwafanya wanafunzi wawe na uwezo wa kujiamini kuongea mbele za watu, kujenga hoja zenye mashiko na kuongeza uwezo wao wa kuzungumza lugha kwa ufasaha hasa kingereza.

Lakini kuna baadhi ya motion kwa upande wangu naona si sahihi.Motion kama " a father is better than a mother" au "A doctor is better than a teacher".Si sahihi kwa watoto hasa shule za msingi na hata sekondari kwasababu haziwajengei watoto uwezo wa kufikiri badala yake kutumia hisia na kubwa zaidi huchagiza dhana potofu.

Kipindi nipo shule ya Msingi,kuna mwanafunzi mwenzetu alisema, "mother is better than a father because my father always beat my mother".Motion kama hizi zinaibua hisia za chuki,hasira au kumbukumbu mbaya miongoni mwa watoto,hali ambayo inaathiri ufanisi wao katika masomo. Na zaidi ya yote motion hizi zimekuwa zikijirudia mara kwa mara.

Kwa nini zisitafutwe motion ambazo zitaongeza uwezo wa wanafunzi kupambanua zaidi matatizo na ugunduzi kuliko kujikita kulinganisha ubora kati ya baba na mama au mwalimu na daktari.
 
FB_IMG_16887121389037936.jpg
 
Back
Top Bottom